Toka mwaka 2009 hadi sasa Diamond Platnumz amekuwa akifanya vizuri kimuziki na kipindi chote hicho ameweza kushinda tuzo za ndani na za kimataifa pia. Kabati lake lina tuzo kubwa zaidi ya 10 kama Channel O Music Video Awards, HiPipo Music Awards, MTV Europe Music Awards/WORLDWIDE ACT AFRICA/INDIA, MTV Africa Music Awards, African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) na nyinginezo. Kwa mwaka huu amefanya mengi makubwa na mazuri ingawa amekuwa na changamoto kubwa kwake.Chini nimeweka yale aliyofanikiwa na yale yalimpatia changamoto kwa huu. 1. Muziki Wake Ni mwaka ambao Diamond Platnumz amejikuta nyimbo zake tatu zikifungiwa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA). Diamond hakuwa msanii wa kufungiwa lakini mwaka huu upepo huo umempuliza vilivyo. February 28, 2018 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea orodha ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA). Nyimbo hizo ni zile ambazo hazikupaswa kuchezwa kwenye vyombo vya habari....