Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya UMOJA WA MATAIFA

Muungano wa G7 na Umoja wa mataifa walaani mapigano mapya Libya

Vikosi tiifu kwa serikali ya Tripoli vimeripotiwa kuungana na serikali kulinda mji mkuu Mataifa yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi duniani G7, pamoja na Umoja wa mataifa yamelaani vikali mapigano yaliozuka upya nchini Libya. Mataifa hayo yanataka pande zinazohasimiana Libya "kusitisha mara moja shughuli za kijeshi". Baraza kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa pia limetoa wito huo. Tripoli ni makao makuu ya serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa, na ambayo pia inaungwa mkono na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Vikosi vya kulinda usalama vya umoja wa mataifa katika mji huo vimekuwa katika hali ya tahadhari. Ghasia zimekumba Libya tangu utawala kiongozi wa nchi hiyo wa mda mrefu, Muammar Gaddafi kuangushwa na yeye kuuawa mwaka 2011. Nini kinachofanyika ? Kamanda Khalifa Haftar, ambaye ni kiongozi wa vikosi vya kijeshi vinavyopinga utawala wa Tripoli siku ya Alhamisi aliamuru vikosi vyake kuingia mji wa Libya. Hatua hiyo ilijiri wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Ma...

Bunge la Umoja wa Ulaya latoa azimio la kulinda haki za binadamu Tanzania

Rais wa Tanzania akiwa na mjumbe wa Umoja wa Ulaya Tanzania, Balozi Roeland van de Geer Bunge la Umoja wa Ulaya limetoa njia iitakayo kwa mustakabali wao juu ya uhusiano kati yao na Tanzania kutokana kile walichokiita kuongezeka kwa ukiukwaji wa haki za binaadamu Tanzania. Azimio hilo limeeleza namna ambavyo hali ya kisiasa nchini Tanzania inavyokandamiza uhuru wa wananchi kutokana na sheria kali zilizopo dhidi ya asasi za kiraia, watetezi wa haki za binadamu, vyombo vya habari na vyama vya siasa na huku hofu kubwa ikitanda kwa wapenzi wa jinsia moja. Vilevile wamekemea matukio yote ya chuki na vurugu dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kuitaka serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa Paul Makonda anaacha kuwatishia watu jamii hiyo na haki kutendeka. Hata hivyoserikali ya Tanzania ilijitenga na msimamo wa kiongozi huyo wa Dar es salaam. Bunge hilo limetaka uchunguzi huru kufanyika ili ukweli juu ya mashambulio na unyanyasaji dhidi ya waandishi wa habari, wapenzi wa jinsia mo...

Mtanzania Joyce Msuya apandishwa cheo UNEP

Mtanzania Joyce Msuya ateuliwa kaimu kiongozi wa shirika la UNEP lenye makao yake Nairobi UN Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amemteua Mtanzania Joyce Msuya kuwa kuwa kaimu kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira, UNEP. Bi Msuya amekuwa Naibu Katibu Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo ambalo lina makao makuu yake jijini Nairobi, Kenya. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amenukuliwa na vyombo vya habari vya kimataifa akisema Antonio Guterres amechukua hatua hiyo huku akiendelea kumtafuta mkuu wa kudumu wa UNEP. Wadhifa wa kiongozi wa UNEP ulikuwa umebaki wazi baada ya kujiuzulu kwa Erik Solheim ambaye amekumbwa na kashfa kuhusu gharama yake ya matumizi katika safari. Mswada wa ripoti ya ukaguzi wa fedha ambayo ilipatikana na gazeti la Uingereza la Guardian, na ambayo BBC imefanikiwa kuisoma, inaonyesha Solheim alitumia jumla ya $488,518 (£382,111) akisafiri siku 529 kati ya siku 668. Alikuwa hayupo afisini kwa t...

Mtanzania Joyce Msuya ateuliwa naibu katibu mkuu wa UNEP

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amemteua Mtanzania Joyce Msuya kuwa Naibu Katibu Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mazingira duniani, UNEP. Afisi kuu za shirika hilo la UN huwa jijini Nairobi, Kenya. Bi Msuya atachukua nafasi ya Ibrahim Thiaw wa Mauritania, ambaye amemaliza muda wake wa kuhudumu. Hadi wakati wa kuteuliwa kwake Jumatatu, Bi Msuya alikuwa mshauri wa Makamu Rais wa Benki ya Dunia kwa ukanda wa Asia Mashariki na Pacific jijini Washington, DC wadhifa alioushikilia tangu mwaka jana. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric, kwa mujibu wa UN alisema "Bi Msuya analeta uzoefu wake wa zaidi ya miaka 20 kwenye nyanja za maendeleo ya kimataifa kuanzia masuala ya mashirika, mikakati, uendeshaji, ufahamu wa usimamizi na ubia alioupata wakati akifanya kazi huko Afrika, Amerika Kusini na Asia." Alishika nyadhifa mbalimbali katika ngazi ya uandamizi kwenye Benki ya Dunia ikiwemo mwakilishi wa Benki ya Dunia na Mkuu wa...

Zarif afanya juhudi za kuokoa makubaliano ya kinyuklia

Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Javad Zarif amesema nchi yake itahitaji uhakikisho kutoka mataifa mengine yenye nguvu  duniani iwapo iendelee kutekeleza mkataba wa kinyuklia wa mwaka  2015, baada ya Marekani  ikujitoa. Waziri wa mambo  ya  kigeni  wa Urusi  Sergei Lavrov  alikutana  na  mwenzake huyo wa  Iran mjini Moscow  Jumatatu  kujadili kile  kinachoweza  kufanyika  kulinda makubaliano  hayo  na  Iran  baada  ya  uamuzi  wa  rais  wa Marekani Donald Trump kujitoa  katika  mkataba  huo.  Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif Iran  jana  iliupa  Umoja  wa  Ulaya  siku  60 kutoa uhakikisho wa kuendelea  na  utekelezaji  wa  makubaliano  hayo  ya  kinyuklia baada...

Shambulio la kemikali nchini Syria: Wachunguzi waruhusiwa kuzuru Douma

Wakaazi wakitembea karibu na eneo lililodaiwa kushambuliwa na kemikali Douma siku ya Jumapili wiki moja baada ya shambulio Wachunguzi wa silaha za kemikali nchini Syria wataruhusiwa kuzuru katika eneo linalodaiwa kushambuliwa na silaha za sumu siku ya Jumatano, kulingana na uUrusi. Kundi hilo la kimataifa limekuwa nchini humo tangu siku ya Jumamosi lakini halijaruhusiwa kuingia Douma. Shambulio hilo la siku ya Aprili 7 lilivutia shambulio dhidi ya serikali ya Syria lililotekelezwa kwa pamoja na Marekani, Uingereza na Ufaransa wiki moja baadaye. Syria na mshirika wake Urusi wamekana shambulio lolote la kemikali huku Urusi ikitaja madai hayo kama 'yaliopangwa'. Mapema siku ya Jumanne , chombo cha habari cha Syria kilisema kuwa ulinzi wa angani wa taifa hilo ulikabiliana na shambulio la makombora juu ya nga ya magharibi mwa mji wa Homs. Makombora hayo yalilenga kambi za wanahewa wa Shayrat lakini haikusema ni nani aliyetekeleza mashambulio hayo. Image cap...

Wafadhili waichangishia fedha Congo

Wafadhili wanakutana mjini Geneva Uswisi Ijumaa katika harakati za kuchangisha dola bilioni 1.7 kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambayo inakabiliwa na mzozo. Wataalam wanasema huenda mzozo huo ukapindukia na kuwa janga kubwa. Mkutano huo unakuja wakati kukiwa na hofu kwamba  mizozo ya kikabila, ufisadi na hali mbaya ya usalama ni mambo yanayozusha hofu ya umwagikaji damu. Kwa wale walioachwa bila makao, kitisho ni cha kweli. Raia mmoja wa Congo alielezea mzozo wa kikabila katika mkoa wa Ituri kwa kusema, "ni kama wakati tulipokuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe." Kulingana na makadirio ya shirika la msalaba mwekundu karibu Wacongo 70,000 wamekimbilia Uganda kwa kuuvuka mto Albert tangu Januari. Ituri ni mkoa mmoja tu kati ya mingi ambayo makundi yaliyojihami na wahalifu wanawasumbua raia. Ukosefu wa usalama umezidisha idadi ya wakimbizi wa ndani ya nchi Zaidi ya hayo kuna mzozo wa kisiasa unaozunguka suala la urais ambapo watu wengi wanamtaka rais Joseph...