Siku ya leo katika pekua pekua zangu za kuongeza chakula cha ubongo nilikutana na kauli ambayo kiukweli ilifanya mishipa yangu ya ardenalini kuweza kushtuka kwa kasi kama vile nimeona kitu cha hatari sana. Kauli hiyo ilikuwa na maneno mawili yenye kubeba ujumbe mzito ambao sina uhakika kama, ujumbe huo upo mzani ambao ataweza kupima kilo zake, hii ni kutokana na uzito uliopo katika ulipo katika ujumbe huo, labda ujumbe huo upimwe na kichwa cha mwanadamu mwenye mtazamo chanya ndio anaweza kuuelewa. Ujumbe huo unasema “unachokiogopa ndicho kitakachokua” narudia kusema tena unachokiogopa ndicho kitakachokua. Kwa haraka haraka unaweza usielewe maana ya msemo huo ila pindi utulizapo fikra ya ujazo wa akili unaweza kuelewa. Binafsi nilichokielewa katika kauli hii ni kwamba, moja kati changamoto kubwa ambayo huwazuia watu wake kutoweza kutimiza makusudio yao hapa dunia ni kitu ambacho tunachokiita ni woga. Woga ndio ambao umekua tatizo...