Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba 26, 2017

Hawaii yafanyia jaribio king'ora cha kuonya shambulizi la nyuklia

MTEULE THE BEST Hawaii yafanyia jaribio king'ora cha kuonya kuhusu shambulizi la nyuklia Kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa vita baridi jimbo la Hawaii nchini Marekani limefanyia jaribio king'ora cha kuonya kuhusu shambulizi la nyuklia Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya jaribio la kombora la masafa marefu lililofanywa na Korea Kaskazini mapema wiki hii. Hawai kawaida ina ving'ora ambavyo huonya kuhusu majanga ya asili kama tsunami. Kingora cha nyuklia kina mlio tofauti ambacho huwaonya watu kusalia manyumbani wakisubiri ushauri zaidi. Lakini king'ora hicho kilisikika tena Ijumaa na kitarudiwa klila jumatatu ya kwanza ya mwezi. Kombora linalorushwa kutoka Korea Kaskazini linaweza kushambulia Hawaii ndani ya dakika 20 baada ya kufyatuliwa. Hivi majuzi Korea ilifyatua kombora mpya la masafa marefu ambalo inadai kuwa linaweza kushambulia ndani ya Marekani. Kombora linalorushwa kutoka Korea Kaskazini linaweza kushambulia Hawaii ndani ya dakika 20 ...

Rais wa TFF ateuliwa ndani ya CECAFA

MTEULE THE BEST Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameshinda nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji katika Baraza la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA). Katika uchaguzi huo uliofanyika leo Desemba 2, 2017 jijini Nairobi, Kenya Rais Karia alipita bila kupingwa baada ya wanachama watatu kati ya nane kujitoa hivyo watano waliobaki kuchaguliwa bila kupingwa. Wajumbe hao ambao wataungana na Rais wa CECAFA, Mhandisi Mutasim Gafar wa Sudan watakuwa na kibarua cha kuboresha utendaji kazi wa baraza hilo kwa ajili ya kuimarisha soka la Afrika Mashariki na kati. Wengine waliochaguliwa ni Abdiqaani Arab Said (Somalia), Aimable Habimana (Burundi), Juneid Basha Tilmo (Ethiopia) na Mwanamke Petra Dorris wa Kenya.

Nasari avamiwa anusurika kupigwa risasi usiku

MTEULE THE BEST Mbunge wa Jimbo la arumeru Mashariki Joshua Nassari, amevamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake Usa River mkoani Arusha, na kunusurika kupigwa na risasi ambazo zimeua mbwa wake. Kwenye ukurasa wake wa twitter Joshua Nassari ameandika ujumbe akitoa taarifa kuwa watu hao walivamia nyumbani kwake usiku wakiwa na silaha za moto ambazo waliwafyatulia mbwa wake, na yeye kunusurika baada ya kukimbia akiwa na mkewe, kitendo ambacho amesema kimemfanya akose imani na nchi yake. "Nimevamiwa nyumbani kwangu maeneo ya Usa River usiku huu na watu wenye silaha, na kufyatua risasi ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nje ya nyumba. Nimefanikiwa kukimbia na mke wangu na kuripoti kituo cha Polisi. Nimekuwa nikitishiwa kuuawa kila siku, sina amani ndani ya nchi yangu", ameandika Joshua Nassari. Kufuatia tukio hilo East Africa Television ilifanya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha kupata taarifa zaidi juu ya tukio hilo, na simu yake kuita bila m...

MPIRA ULIVYOBADILISHA MAISHA YA MASTAA 10 HIZI NDO NYUMBA WALIZO KUWA WANAISHI NA ZA SASA 10 Footballers Houses - Then and Now - Ronaldo, Neymar, Messi and

MTEULE THE BESTBEST 10 Goals the Football World will Never Forget_HDHD Magoli bora zaidi duniani angalie hapa MPIRA ULIVYOBADILISHA MAISHA YA MASTAA 10 HIZI NDO NYUMBA WALIZO KUWA WANAISHI NA ZA SASA  Rooney, benzema, messi, Neymar, Ronald  na wengine  angali a mijengo yao ANGALIA HAPA

Mwana michezo unaikumbuka haya TOP 10 GOALS- 2014 FIFA World Cup Brazil™ [OFFICIAL]_HIGH TUKUTANE RUSSIA 🇷🇺 2018

MTEULE THE BEST Magoli 10 bora final za world 🌏  cup 2014 angalia hapa chino

Manula aitumia salamu Libya

MTEULE THE BEST Mlinda mlango wa Timu ya Taifa ya Tanzania Bara “Kilimanjaro Stars” Aishi Salum Manula amesema kutokuwajua vizuri wapinzani wao Timu ya Taifa ya Libya hakutakuwa chanzo cha kutokufanya vizuri katika mchezo wa awali wa michuano ya CECAFA Challenge nchini Kenya. Manula amesema mara nyingi Kocha hutoa mbinu kwa wachezaji wake kutokana na kuijua japo sio kwa undani timu wanayokutana nayo hivyo wanaamini Kocha anaifahamu Libya na mbinu walizofundishwa zitawasaidia kuweza kupambana nao ili kuibuka na ushindi katika mchezo huo na inayofuata. " Timu ya Libya siijui kwa hivyo lakini nadhani kwa vile ambavyo Mwalimu amatufundisha na mbinu ambazo ametupa kuelekea katika mchezo wetu wa kwanza nadhani tutafanikiwa kwani nadhani yeye ameweza kuifuatilia vizuri zaidi na kwaundani na kujua kwamba Libya ipo vipi ili atupatie mbinu gani na tuweze kuushinda mchezo huo , " amesema. Aishi ameongeza kwa kuwataka watanzania kuendelea kuwapa sa...

Wema Sepetu aondoka rasmi Chadema

Muigizaji wa filamu za kibongo na Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu ametangaza rasmi kurudi Chama Cha Mapinduzi huku akidai kwamba hawezi kuishi kwenye nyumba inayomkosesha amani. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema Sepetu amesema kwamba anatangaza rasmi kuondoka ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambacho alitangaza kujiunga nacho Februari mwaka huu "Siwezi Kuendelea kuishi kwenye nyumba inayo nikosesha amani... Peace of mind is everything for me. Natangaza rasmi kuondoka Chadema na kurudi nyumbani" . Wema Sepetu. 

NEYMAR JR NIMEJITOA KWA TAIFA LANGU

MTEULE THE BEST Nyota wa Brazil Neymar Jr amesema atajitoa kwa uwezo wake wote kuhakikisha taifa lake linashinda Kombe la Dunia mwaka 2018 kwenye fainali zitakazofanyika nchini Urusi. Kikosi chetu kwasasa ni bora tofauti na ilivyokuwa mwaka 2014 tuliposhindwa kuchukua ubingwa tukiwa nyumbani, nitacheza kwa uwezo wangu wote kuhakikisha tunarejesha heshima ya kutwaa ubingwa wa dunia”, amesema Neymar. Nyota huyo anayechezea PSG ya Ufaransa ameongeza kuwa timu yao ni bora ndio maana ilipoteza mechi moja tu kwenye michuano ya kuwania kufuzu fainali hizo kupitia kundi la Amerika ya Kusini (CONMEBOL). “Kufuzu kwa kupoteza mechi moja tu kwenye kundi gumu la CONMEBOL ni hatua nzuri na imetufanya tujiamini na tutafanya vizuri na hayatajirudia mambo yaliyotokea kwenye fainali za miaka minne iliyopita”. Kwenye fainali za Kombe la Dunia 2014, Brazil iliondolewa kwenye hatua ya nusu fainali baada ya kukubali kichapo cha mabao 7-1 kutoka kwa Ujerumani ambayo iliibuka bingwa wa dunia ...

TFF YA TOLEA MAELEZO HOJA YA ZITTO

MTEULE THE BEST Shirikisho la Soka Tanzania TFF limejibu hoja iliyotolewa na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, kuitaka Tanzania isusie kucheza mechi na Libya ili kupinga vitendo vya biashara ya utumwa inayoendelea nchini humo. Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema suala hilo limefikishwa kwa uongozi wa TFF na litatolewa majibu hivi karibuni. "Msimamo utatolewa na viongozi wangu mara baada ya kukaa na kutafakari hali halisi kwa sasa, na wenye uwezo wa kukaa na kutafakari ni viongozi wa juu, itakapokuwa tayari mtajulishwa", amesema Alfred Lucas. Hapo jana Zitto Kabwe ametoa wito kwa TFF kuitaka timu ya Kilinajaro Stars isusie mechi inayotarajiwa kuchezwa na Libya, ili kuonyesha kutokubaliana na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuendeleza biasha ra utumwa.

Trump: Tutaiangamiza Korea Kaskazini iwapo vita vitazuka

MTEULE THE BEST Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un na mwenzake wa Marekani Donald Trump Marekani imeyataka mataifa yote kukatiza uhusiano wa kidiplomasia na ule wa kibiashara na Korea Kaskazini baada ya taifa hilo kufanyia jaribio la kombora lake la masafa marefu. Akizungumza katika baraza la usalama la umoja wa kimataifa ,mjumbe wa Marekani katika baraza hilo Nikki Haley amesema kuwa rais Trump amemtaka mwenzake wa China kukata usambazaji wa mafuta kwa Pyongyang. Amesema kuwa Marekani haitaki mzozo lakini Korea Kaskazini itaangamizwa iwapo vita vitazuka. Onyo hilo linajiri baada ya Pyonyang kufanyia majaribio kombora lake la kwanza katika kipindi cha miezi miwili. Korea Kaskazini imesema kuwa kombora hilo lililorushwa siku ya Jumatano ambalo inasema liliruka kimo cha kilomita 4,475, ikiwa ni mara kumi zaidi ya kimo cha kituo cha angani. Madai hayo hayakuthibitishwa na wataalam wametiliashaka uwezo wa taifa hilo kuwa na teknolojia kama hiyo. Hatahivyo kiongo...

WAZIRI MKUU AMPA SIRO KIRUNGU CHA KUWAKAMATA WA FANYA BIASHARA WALIOTUMIA JINA LA WAZIRI MKUU

🇹🇿 Tanzania  waziri mkuu atoa amri kukamatwa kwa wafanyabiashara kwa kutumia jina lake kwa kukwepa kodi  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ina madhumuni ya Mkaguzi Mkuu wa polisi Simon sirro kumkamata wamiliki wa nas kampuni na ile ya wallmark kwa inadaiwa kujaribu kutumia jina lake kwa wazi 44 trailers kutoka Dar es Salaam bandari katika hoja yenye lengo la kukwepa kutokana kodi. pia kwa madhumuni ya bandari Tanzania mamlaka (TPA) madhubuti kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu badala ya kusikiliza wafanyabiashara, ambaye wakati mwingine kutumia majina ya juu ya viongozi wa serikali ya kujaribu na ya wazi yao ya mizigo. "unapaswa si kuruhusu mtu kuja hapa na kuwaambia kwamba amekuwa ilivyoagizwa na Rais au Makamu wa Rais au Hata mimi wazi yake ya mizigo. unapaswa daima fimbo na sheria na taratibu," alisisitiza Mr Majaliwa. yeye alitoa agizo siku ya Jumatano, Novemba 29, wakati yeye alifanya impromptu ziara ya bandari. kwa mujibu wa Waziri Mkuu, wafanyabi...

Viongozi wa Ulaya wakutana na wenzao wa Afrika Abidjan

Viongozi kutoka Ufaransa, Ubeigiji, Luxemburg, wote wakiwa ni viongozi wa kiume wenye umri unaokurubia miaka 40 wanajaribu kujitenganisha na picha ya wakoloni wa zamani wa Afrika, wakitetea umuhimu wa kuendeleza biashara na kuwekeza katika miradi ya maendeleo na usalama barani humo pamoja na kushughulikia vyanzo vya uhamaji. Uhamaji ndio mada kuu katika mkutano huu wa kilele mjini Abidjan, mji mkuu wa kibiashara wa Côte d'Ivoire, mada iliyopata nguvu kutokana na kanda ya video iliyotangazwa hivi karibuni na kituo cha televisheni cha CNN  na kuonyesha jinsi vijana wa kiafrika walivyokuwa wakiuzwa kama watumwa katika masoko ya mnada nchini Libya. Akizungumza kuhusu kisa hicho cha karaha, kansela Angela Merkel amesema:"Mada ya uhamaji kinyume na sheria inakamata nafasi muhimu katika bara lote la Afrika wakati huu tulio nao kwasabau kuna rirpoti zinazosema vijana wa kiafrika wamekuwa wakiuzwa kama watumwa nchini Libya. Na hiyo ndio sababu mada hiyo inazusha jazba kubwa kati...

Everton wanakaribia kumteua Allardyce kuwa meneja na West Brom wamteua Pardew kuwa Meneja

Uteuzi wa Alan Pardew (kulia) una maana kwamba sasa yeye na Tony Pulis wamekuwa wakufunzi wa West Brom na Crystal Palace Ligi ya Premia West Brom wamemteua meneja wa zamani wa Newcastle na Crystal Palace Alan Pardew kuwa meneja wao mpya. West Brom walimfuta kazi Tony Pulis mnamo 20 Novemba baada yao kucheza mechi 10 Ligi ya Premia bila kushinda mechi hata moja. Walikuwa alama moja pekee juu ya eneo la kushushwa daraja. Pardew, 56, amekuwa bila kazi tangu alipofutwa na Crystal Palace Desemba 2016. Ametia saini mkataba wa kudumu hadi msimu wa 2019-20, na sasa amekuwa meneja wa sita kuteuliwa Albion tangu 2011. "Nimefurahishwa sana na fursa hii ambayo nimepewa na Albion na nasubiri kwa hamu kuanza kazi na kikosi ambacho ninaamini kina wachezaji wenye vipaji sana," Pardew amesema. "Kibarua cha kwanza kitakuwa kupata matokeo yatakayotuinua kwenye jedwali." Mechi yake ya kwanza usukani itakuwa dhidi ya Palace ligini uwanjani Hawthorns Jumamosi, 2 Desemba (15:00 ...

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 29.11.2017

David Luiz Real Madrid wanalenga kumsajili beki wa Chelsea na Brazil David Luiz 30 ambaye hatakikani katika uwanja wa Stamford Bridge msimu huu. (Daily Mail) Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte anasema kuwa hajaelezwa iwapo atalazimika kuwasajili wachezaji wowote katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari iwapo mabingwa hao watetezi wanatarajiwa kuwafikia viongozi wa ligi Manchester City. (Guardian) Leroy Sane Mchezaji wa Manchester City na raia wa Ujerumani mwenye umri wa 21 Leroy Sane atapewa kandarasi mpya na Manchester City mwishoni mwa msimu huu. (Sun) Watford wameonya kwamba mshambuliaji wao raia wa Brazil Richarlison, 20, ambaye alijiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitano kutoka Fluminence mnamo mwezi Agosti kwa kitita cha £11m na anavutia klabu za Tottenham na Chelsea hauzwi wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (London Evening Standard) Alexandro Sane Chelsea wanatarajiwa kumnunua beki wa Juventus Alex Sandro ,26, mwezi Januari baada ya k...

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 21.11.2017

MTEULE THE BEST Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola analenga kumnunua Riyad Mahrez katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari (Don Balon via The Sun) Riyad Mahrez Nahodha wa zamani wa klabu ya West Brom Derek McInnes, anayeisimamia Aberdeen, ni miongoni mwa wagombea wa kuchukua mahala pake mkufunzi wa klabu hiyo aliyefutwa kazi Tony Pulis kama mkufunzi. (The Scottish Sun) Hatahivyo mashabiki wa West Brom wanamtaka mkufunzi wa zamani wa Everton kuchukua mahala pake Pulis. (Express & Star) Mkufunzi wa zamani wa klabu ya West Ham Alan Pardew, meneja wa zamani Nigel Pearson na mkufunzi wa timu ya Ireland Martin O'Neill ni miongoni mwa wakufunzi walioorodheshwa katika kuchukua kazi ya meneja wa West Brom job. (Guardian) Sam Allardyce Mkufunzi wa zamani wa Uingereza Sam Allardyce pia analengwa kuichukua kazi ya ukufunzi wa klabu ya West Brom na imebainika kwamba baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo walikuwa wakitaka mkufunzi Pulis kuondoka. (Mirror) Puli...

Wachezaji watatu waongezwa Kilimanjaro Stars

MTEULE THE BEST Kocha Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Ammy Conrad Ninje, ameongeza nyota watatu katika kikosi chake baada ya Baraza la Soka la Afrika Mashariki (CECAFA), kuridhia kuongezwa wachezaji watatu kwa kila timu. Awali CECAFA ilihitaji wachezaji 20 tu, lakini sasa wameongeza watatu na kufanya idadi mpya ya wachezaji watakaoshiriki michuano hiyo ya Chalenji kwa mwaka huu kuwa 23. Wachezaji walioongezwa ni Kipa Ramadhani Kabwili kutoka Yanga, Amani Kiata wa Nakuru All Stars ya Kenya na Yahya Zayd kutoka Azam FC. Wachezaji 20 walioitwa awali na kocha Ninje ni makipa Aishi Manula (Simba SC) na Peter Manyika (Singida United). Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphace Maganga (Mbao FC), Kelvin Yondani (Young Africans), Kennedy Juma (Singida United), Erasto Nyoni (Simba SC) na Mohammed Hussein (Simba SC). Viungo wa kati ni Himid Mao ambaye ni Nahodha (Azam FC), Jonas Mkude (Simba SC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mza...

Korea Kaskazini yarusha kombora la masafa marefu lenye nguvu zaidi kupita yote duniani

MTEULE THE BEST Korea Kaskazini imesema imefanikiwa kufanya jaribio la kombora la masafa marefu ambalo lina nguvu ya kushambulia eneo lolote Marekani. Jumuiya ya kimataifa imelaani vikali kurushwa kwa kombora lijulikanalo Hwangsong 15. Jaribio hilo ndilo la kwanza kurushwa na Korea Kaskazini tangu mwezi Septemba na linakuja wiki moja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuiweka nchi hiyo katika orodha ya nchi zinazotajwa kuuunga mkono ugaidi. Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis amesema kombora hilo la hivi punde limeruka umbali mrefu zaidi na hivyo kumaanisha kuwa Korea Kaskazini inazidi kujiimarisha katika majaribio yake ya makombora. Kombora hilo la masafa marefu linasemekana kuruka juu na mbali zaidi kuliko makombora yaliyofanyiwa marekebisho kipindi cha nyuma. Kombora lina nguvu kuliko yaliyopita Kulingana na taarifa iliyosomwa katika kituo cha televisheni cha Korea Kaskazini, Kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un alishuhudia kurushwa kwa ufanisi kombora hilo ...

Manchester United yaichapa Watford 4-2

MTEULE THE BEST Ashley Young alionyesha kiwango kizuri kwenye mchezo huo Manchester United ikiwa ugenini katika dimba la Vicarage Road imefanikiwa kuichapa Watford 4-2 katika ushindi ambao awali ulionekana kuwa mgumu kwa United kabla ya kuanza kwa mchezo. Magoli ya United yamefungwa na Ashley Young akiingia nyavuni mara mbili huku Antony Martial akipachika goli la tatu na Jesse Lingard. Troy Deeney na Doucaure walindika magoli mawili ya Watford. Meneja wa Manchester United José Mourinho amesema ushindi huo utaongezaotisha kwa timu yake. Wachezaji wa Watford wakishangilia Man United inasalia nafasi ya pili ikiwa na alama 32 ikiwa ni alama tano nyuma ya Man City ambayo pia ina mchezo mmoja mkononi.

ZITTO AFUNGUKA JUU YA RAIS KUTOENDA KENYA NA MAKAMU KUPOKELEWA NA BALOZI

MTEULE THE BEST Zitto Kabwe amefunguka na kusema kitendo cha Makamu wa Rais Mhe. Samia kupokelewa na Balozi Kenya ni ishara kuwa mahusiano ya Tanzania na Kenya hayapo vizuri na kudai Rais Magufuli kutokwenda kwenye sherehe za kuapishwa Kenyatta inaweza kueleweka. Zitto Kabwe amesema hayo kupitia mtandao wake wa twitter na kusema kitendo cha Rais Magufuli kutohudhuria kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta inaweza kueleweka kwani kiongozi huyo hakuweza kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame. "Makamu wetu wa Rais kupokelewa na Balozi ( sio hata Waziri wa Mashauri ya Kigeni au Waziri mwengine) ni dalili kuwa mahusiano yetu yanalega lega. Rais kutokwenda Kenya inaweza kueleweka maana hata Rwanda hakwenda kwenye uapishaji wa Paul Kagame" aliandika Zitto TAARIFA ZAIDI MAGUFULI  Rais John Pombe Magufuli Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amemtuma makamu wake wa rais kumwakilisha katika sherehe ya kua...

Wanawake ambao ni wa Freemason na itikadi zao

Wanawake wa Freemason wamekuwa wakikongamana kwa zaidi ya miaka 100 sasa - wakifanya matambiko na sherehe sawa na wenzao wa kiume. Lakini si watu wengi wanaofahamu kuwepo kwa kundi hili. Sasa tunaweza kukufahamisha zaidi kuhusu shughuli za Freemason hawa wa kike baada ya kipindi cha redio cha Victoria Derbyshire cha BBC kuruhusiwa kuzungumza nao. "Freemason ni nani?" anauliza mmoja wa viongozi wao ambao huitwa master (gunge) katika Kongamano Tukufu la Jumuiya ya Freemason wa Kale. "Ni mfumo wa kipekee wa maadili ambao umezingirwa na istiari na ishara zenye maana," anajibu Dialazaza Nkela. Nkela anashiriki katika sherehe ya kipekee ya kumfikisha ngazi ambayo hufahamika kama "shahada ya pili". Ni sherehe ya kusherehekea kupanda hadhi kwake katika kundi lake. Kufikia kwake "shahada ya kwanza" kuliadhimishwa kwa kuingizwa kwake katika kundi hilo, shughuli ambayo ilihusisha yeye kuweka wazi "mkono wake wa kulia, ziwa lake la kulia na goti l...

Ulinzi mkali Nairobi Kenyatta akitarajiwa kuapishwa

Ulinzi umeimarishwa katika jiji kuu la Kenya, Nairobi pamoja na miji mingine mikuu Rais Uhuru Kenyatta akitarajiwa kuapishwa kuongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine hapo kesho. Muungano wa upinzani umetangaza kwamba hautambui sherehe hiyo na haumtambui Bw Kenyatta kama rais aliyechaguliwa na wananchi. Kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga amepanga kuandaa mkutano mkubwa wa kuwakumbuka watu waliofariki wakati wa makabiliano kati ya wafuasi wa upinzani na polisi. Bw Odinga na muungano wake wa National Super Alliance (Nasa) wamesisitiza kwamba mkutano huo utafanyika katika uwanja wa Jacarada, Nairobi, takriban kilomita kumi hivi kutoka uwanja wa Kasarani ambapo sherehe ya kuapishwa kwa Bw Kenyatta itakuwa inaendelea. Polisi hata hivyo wamesisitiza kwamba hakutakuwa na mkutano mwingine Nairobi ila sherehe ya kumuapisha Bw Kenyatta. Bw Odinga alisusia uchaguzi wa marudio uliofanyika 26 Oktoba baada ya kufutiliwa mbali kwa uchaguzi wa kwanza uliokuwa umefanyika tarehe 8 Agosti. Mahakam...

Mugabe apewa sikukuu ya taifa Zimbabwe

Haki miliki ya pichaAFPImage captionMugabe alikuwa ameongoza Zimbabwe tangu uhuru 1980 Serikali ya Zimbabwe imetangaza siku kuu mpya ya kukumbuka mchango wa Robert Mugabe ambaye aliondolewa madarakani wiki iliyopita. Gazeti la serikali la Herald limesema sikukuu hiyo itakuwa ikiadhimishwa siku ya kuzaliwa kwa Bw Mugabe kila mwaka. Uamuzi wa kusherehekea Siku ya Taifa ya Vijana ya Robert Gabriel Mugabe kila 21 Februari ulifanywa rasmi kupitia tangazo rasmi kwenye gazeti la serikali. Mugabe: Mambo 5 unayopaswa kuyafamu Mugabe huwa anapumzisha macho si kulala Je Robert Mugabe ni nani? Tangazo hilo lilichapishwa Ijumaa - siku ambayo Rais Emmerson Mnangagwa aliapishwa kuwa rais, na kufikisha kikomo uongozi wa Mugabe wa miaka 37. Serikali ya Bw Mugabe ilikuwa imeamua kutangaza siku ya kuzaliwa kwake kuwa sikukuu ya taifa mwezi Agosti, baada ya kampeni kutoka kwa mrengo wa vijana katika chama cha Zanu-PF. Image captionRaia walimshangilia rais Mpya wa Zimbabwe E...

HUMPHREY POLEPOLE LEO KWENYE PRESS CONFERENCE.*

*NUKUU ZA NDG. HUMPHREY POLEPOLE LEO KWENYE PRESS CONFERENCE.* Tarehe 27/11/2017. "Chama Cha Mapinduzi tulikaa na tulifanya mafunzo kwa watumishi wetu wote kwenye ngazi na maeneo ambazo tunafanya uchaguzi" Ndg  Humphrey Polepole. "Wagombea wetu pahala pote walijinasibu kuuza na kufafanua ilani ya uchaguzi". Ndg. Humphrey Polepole "Kwa vyama vya siasa, Ukiona hoja zako zinafanyiwa kazi na serikali unatakiwa kufurahi na siyo kuhujumu" Ndg. Humphrey Polepole. "Wagombea wote wa Chama Cha  Mapinduzi waliimba ilani ilani". Ndg. Humphrey Polepole "Wanachama wa Chama cha Mapinduzi walishiriki kujipanga" Ndg. Humphrey Polepole "Chama kikaelekeza mikoa yenye uchaguzi kufanya siasa ya kisayansi siasa inayoshughulisha na shida za watu" Ndg. Humphrey Polepole "Kampeni hizi kimsingi zimefanyiwa kazi na viongozi wa Mikoa wa Chama Cha Mapinduzi" Ndg. Humphrey Polepole. "Katika siku mbili za mwisho tulipeleka vio...

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)                                                   TAARIFA KWA UMMA

 SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)                                                   TAARIFA KWA UMMA Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) unawafahamisha Wateja wake wote na Wananchi kwa ujumla kuwa; TANESCO  imeanza utekelezaji wa  Agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli, kuhusu kubomolewa  kwa Jengo la Ofisi za TANESCO  Makao Makuu, liliopo Ubungo Jijini Dar es salam. Kuanzia Jumatatu Novemba 27, 2017. Ukuta wa mbele ya jengo umesha vunjwa ,  pia  baadhi ya Watumishi wa Shirika wameanza kuhamishiwa katika Ofisi nyingine za TANESCO zilizopo jijini Dar es salaam ili kupisha shughuli za ubomoaji kufanyika kwa usalama  zaidi. Uongozi w...

Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spika wa bunge la Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai ameongoza  mamia ya wakazi wa Songea mkoani Ruvuma kwenye mazishi ya aliyekuwa  mbunge wa jimbo la Songea  mjini marehemu Leonidas Gama aliyefariki Novemba 23 nyumbani kwake Likuyufusi  mjini Songea.

Wanasayansi: Ziwa Victoria lipo hatarini kukauka Wanasayansi wanasema kwamba ziwa kubwa zaidi lenye maji tulivu barani Afrika Victoria

Wanasayansi: Ziwa Victoria lipo hatarini kukauka Wanasayansi wanasema kwamba ziwa kubwa zaidi lenye maji tulivu barani Afrika Victoria linalounganisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, lipo katika hatari kubwa ya kukauka Muonekano wa ziwa Victoria Wanasayansi wanasema kwamba ziwa kubwa zaidi lenye maji tulivu barani Afrika Victoria linalounganisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, lipo katika hatari kubwa ya kukauka. Wanasema kwamba uvuvi haramu na uliopitiliza pamoja na uvamizi wa mazingira kuzunguka maeneo ya ziwa ni sababu kubwa. Maji machafu pia yanayotiririshwa kuelekea kwenye ziwa yanahatarisha usalama wa viumbe vya majini. Mwandishi wa BBC anasema jeshi la Uganda limeweka mipango maalum ikiwa ni pamoja na kuharibu nyenzo za uvuvi zinazotajwa kuwa miongoni mwa sababu.

Bondia, Ibrahim Class wa Tanzania

Bondia, Ibrahim Class wa Tanzania  amepeperusha vyema bendera ya taifa baada ya kutetea ubingwa wake wa dunia katika uzito Mwepesi kwa kumtandika Koos Sebia wa Afrika kusini kwa alama katika pambano lilofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam . Mgeni rasmi katika pambano hilo alikuwa Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, ambaye amewataka vijana kote nchini kujiandaa vyema kabla ya kushiriki mchezo wowote  kama wanataka kushinda kama alivyofanya Ibrahim Class. Kwa upande wake Ibrahim Class amesema,ataendelea kucheza kwa bidii katika mapambano yake ili aendelee kutamba katika anga za kimataifa.

Papa aizuru Myanmar inayotuhumiwa kwa mauaji Ziara hii huenda ni jukumu zito kidiplomasia katika miaka minne ya Papa Francis kama kiongozi wa kanisa katoliki.

Papa Francis aliondoka Roma Jumapili usiku Papa Francis anaanza ziara ya wiki nzima nchini Myanmar na Bangladesh leo Jumatatu, wakati wasiwasi unaendelea wa kimataifa kuhusu usalama na ulinzi kwa wasilamu wa Rohingya. Anatarajiwa kukutana na Aung Sun Suu Kyi na mkuu wa jeshi Myanmar. Hata kabla ya kuondoka Roma, Papa Francis alikuwa anakabailiwana kitendawili cha kidiplomasia: iwapo kuliita kundi dogo la waislamu Myanmar - Rohingya. Ni jina lisilo tumika na serikali ya kiraia na jeshi - wakieleza kuwa ni wahamiaji haramu kutoka Bangladesh na kwahivyo hawapaswi kuorodheshwa kama mojawapo ya makabila nchinihumo. Nchi hiyo yenye idadi kubwa ya maBudda inajitayarisha kumkaribisha Papa Lakini mashirika ya kutetea haki za binaadamu wanamuomba awaite hivyo, yakieleza kuwa nilazima Papa Francis aoneshe huruma kwa watu walionyimwa uraia na tangu Agosti wamekabiliwa na kile kamishna wa haki za binaadamu katika Umoja wa mataifa amekitaja kuwa 'kinachoonekana kuwa mauaji ya kikabila...