*NUKUU ZA
NDG. HUMPHREY POLEPOLE LEO KWENYE PRESS CONFERENCE.*
Tarehe 27/11/2017.
"Chama Cha Mapinduzi tulikaa na tulifanya mafunzo kwa watumishi wetu wote kwenye ngazi na maeneo ambazo tunafanya uchaguzi" Ndg Humphrey Polepole.
"Wagombea wetu pahala pote walijinasibu kuuza na kufafanua ilani ya uchaguzi". Ndg. Humphrey Polepole
"Kwa vyama vya siasa, Ukiona hoja zako zinafanyiwa kazi na serikali unatakiwa kufurahi na siyo kuhujumu" Ndg. Humphrey Polepole.
"Wagombea wote wa Chama Cha Mapinduzi waliimba ilani ilani". Ndg. Humphrey Polepole
"Wanachama wa Chama cha Mapinduzi walishiriki kujipanga" Ndg. Humphrey Polepole
"Chama kikaelekeza mikoa yenye uchaguzi kufanya siasa ya kisayansi siasa inayoshughulisha na shida za watu" Ndg. Humphrey Polepole
"Kampeni hizi kimsingi zimefanyiwa kazi na viongozi wa Mikoa wa Chama Cha Mapinduzi"
Ndg. Humphrey Polepole.
"Katika siku mbili za mwisho tulipeleka viongozi wetu wa chama kuongeza nguvu" Ndg. Humphrey Polepole.
"Watu ambao tumewapeleka wanarekodi nzuri ya kushughulika na shida za watu huko wanakotoka"
Ndg. Humphrey Polepole.
"Tutizame matokeo ya uchaguzi ya 2015, uchaguzi wa Januari 2017 na Uchaguzi huu wa Sasa" Ndg. Humphrey Polepole.
"Zoezi la uchaguzi lina kabla ya uchaguzi, siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi" Ndg. Humphrey Polepole.
"Vyama vyote vimeshiriki kampeni kuanzia siku ya kwanza hadi ya mwisho kikamilifu"
Ndg. Humphrey Polepole.
"Katika maeneo yote uchaguzi ulienda vizuri"
Ndg. Humphrey Polepole.
"Ilipofika saa6 kiongozi wa upinzani akasema uchaguzi unaendelea vizuri, lisaa limoja baadae kasema kauli nyingine na kuweka mpira kwapani,
Kitendo hichi kinaonesha hakuna ukomavu wakisiasa kwenye siasa za vyama vya upinzani" Ndg. Humphrey Polepole
"Mwanachama wetu akipigwa atumposti mitandaoni tunakwenda polisi kuripoti, na matukio yote tumeyaripoti kwenye vituo vya polisi" Ndg. Humphrey Polepole.
"Tunamuomba na kumsihi sana msajili wa vyama vya siasa atazame mambo haya, na mamlaka zichukue hatua". Ndg. Humphrey Polepole
"Katika kata zote 43 upinzani wameambulia kata moja ya Ibighi Rungwe" Ndg. Humphrey Polepole
"Roho imetuuma sana kupoteza hiyo kata moja, tunafuatilia kama kuna Hujuma tutakata Rufaa.
Tunataka zitimie zote 43." Ndg.Humphrey Polepole.
"Karibia nusu ya Mabaraza ya madiwani halmashauri ya hai walituomba kuhamia CCM" Ndg. Humphrey Polepole.
"Kwanini maeneo ya Arusha na Arumeru wa ambiwe wakatae uchaguzi na zile zingine kote nchi nzima wasikatazwe" Ndg. Humphrey Polepole.
"Kuwaletea watu maji, haija kupiga watu mawe, kuwaletea watu barabara haitaji kuwapiga watu bisibisi" Ndg. Humphrey Polepole.
"Kule singida tumeweka mitambo tutakapoanza kurusha matangazo basi tutasikika vizuri" Ndg. Humphrey Polepole
"2019, 2020 usishangae kuna sunami linakwenda kutokea ambalo halijawahi kutokea" Ndg. Humphrey Polepole
"Wenzetu wanakimbilia mitandaoni Mimi niliposhambulia Mbweni nilikwenda polisi, hatukutaka kura za huruma" Ndg. Humphrey Polepole
Imetolewa na;
Idara ya Itikadi na Uenezi
CHAMA CHA MAPINDUZI.
MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.
Maoni