Air Tanzania: Faida ikoje baada ya kufufuliwa shirika la ndege Tanzania? Ndege ya Dreamliner ilipowasili Tanzania Julai 2018 Wiki hii shirika la ndege nchini- Air Tanzania linaidhinisha njia mpya ya usafiri - jambo linalotazamwa kuwa fursa ya ukuwaji linapokuja sula la usafiri wa abiria. Rais John Pombe Magufuli aliahidi kwamba shirika hilo litaimarishwa na ndege mpya kununuliwa mara baada ya kuingia madarakani. Tanzania, kama ilivyo kwa nchi nyingine kama Zambia, Zimbabwe, Nigeria na Uganda, imelifufua shirika lake la ndege, ama kama lijulikanavyo, Air Tanzania. Uwekezaji mkubwa umefanywa mpaka sasa katika kulifanikisha hilo. "Shirika letu la ndege lilikuwa na hali mbaya sana, lilikuwa na ndege moja tu tena ilikuwa inafanyiwa matengenezo mara kwa mara, soko la ATCL lilishuka sana hadi kufikia asilimia 2.5. Lakini sasa tumenunua ndege 7, na nyingine kubwa aina ya Boeing 787-8 Dreamliner itakuja mwaka 2020", alisema Rais Magufuli mwaka jana 2018 katika hafla ya ...