Modesta Joseph,mwanafunzi aliyeanzisha "Our cries" fursa inayompa mwanafunzi kushtaki anapokutana na unyanyasaji kwenye usafiri anapoenda shule
Madai ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya walimu na wanafunzi katika shule za Nigeria huwa zinachukua vichwa vya habari vya magazeti mengi nchini humo lakini taarifa hizo huwa hazina muendelezo wowote wa hatua gani zimechukuliwa dhidi ya kesi hizi .
Mwaka 2016,wasichana katika shule moja ya bweni mjini Lagos waliacha kufanya mtihani na kuandamana kupinga unyanyasaji wa kijinsia kutoka kwa mwalimu wa kiume.
Jambo ambalo watu wote walivumilia tabia kama hizo miaka ya nyuma waliwaunga mkono.
Mara nyingi wanafunzi wanakuwa hawapo kwenye nafasi ya kujitetea wanapokutana na wanyanyasaji kutokana na mila na desturi za kukaa kimya na kuheshimu waliokuzidi umri.
Hali ambayo ni tofauti kwa binti mdogo kutoka Tanzania ,Modesta Joseph mwenye umri wa miaka 15 ambaye aliamua kutengeneza fursa kwa wanafunzi nchini mwake kutoa taarifa juu ya unyanyasaji.
Modesta anasema wanafunzi wengi jijini Dar es salaam wanakumbana na unyanyasaji kwenye upande wa usafiri wa daladala unaowatoa nyumbani mpaka shule.
Mara nyingi abiria huwa wanagombania kupanda dalada
Wanafunzi nchini humo huwa wanalipa fedha pungufu ya kiwango anacholipa mtu mzima hivyo kuwafanya madereva na wasaidizi wao kuona kuwa ni haki yao kuwanyanyasa na kuwazuia wasiingie kwenye daladala zao ambazo huwa zinakuwa zinagombaniwa na idadi kubwa ya watu.
Gharama ya nauli kwa wanafunzi kuwa tofauti na watu wazima ni changamoto kubwa kwa wanafunzi hao maana wenye gani uona kuwapakiza wanafunzi hao ni hasara.
Wanafunzi wengi hushindwa kuwahi darasani licha ya kuwa walifika mapema katika vituo vya daladala na kupambana kwa masaa kadhaa mpaka kupata usafiri.
"Mara nyingine ,kondakta huwa wanatupiga ,ukiwa ndani ya daladala wanaweza kukushika popote muda wowote wanaojisikia,yaani huwa wanawashika kingono",Modesta aeleza.
Wanafunzi uchelewa shule kwa kukosa usafiri
"Wanaweza hata wakakusuma wakati gari linaenda,siku moja rafiki yangu alifanyiwa hivyo,Wengine hupata hata majeraha wakati wanapogombania kuingia katika basi
na mara nyingi watu wazima huwa hawafanyi chochote zaidi yakuangalia tu".aliongeza Modesta
Fursa hiyo aliyotengeneza Modesta ili kusaidia wanafunzi kutoa taarifa dhidi ya unyanyasaji wa wanafunzi inayoitwa "Our cries" imewapa fursa kwa wanafunzi hao kutuma ujumbe mfupi wa simu au kutumia mtandao wa kijamii ili kutoa malalamiko yao na kwa wale wasiokuwa na simu,kuna boksi kadhaa zimewekwa kwenye shule za sekondari jijini humo.
Jitihada hizi zinashirikiana na mamlaka ya usafirishaji Tanzania inayojulikana kama Sumatra ambao wanafanya kazi na polisi ili kuhakikisha kuwa malalamiko yanayopelekwa yanafanyiwa kazi kwa wakati.
Mlalamikaji anaweza kuandika jina lake au asiandike lakini lazima wataje namba za gari,na daladala hilo lilikuwa linatoka wapi kwenda wapi na kutoa maelezo ya kilichotokea.
Semina mbalimbali zinatolewa kwenye shule za sekondari
Kampeni hiyo ilianzishwa tangu mwaka 2014 na sasa wamepokea mamia ya malalamiko na tunashukuru hata kwa stika ambazo tuliziweka kwenye madaladala na semina ambazo tunaendelea kuzifanya kwenye shule kuhusu kubadili mitazamo kwa wanafunzi maana kuna wengine wanaoona kuwa ni sawa kwa wao kufanyiwa vitendo hivyo vya unyanyasaji.
Modesta anafurahi kuona matokeo chanya ya kampeni hiyo ya Our cries yaani kilio chetu.Kuna baadhi ya wahudumu wa daladala hizo wameshaadhibiwa na Sumatra na polisi.
Anasema hata abiria wameacha kukaa kimya ,wameanza sasa kulalamika wakati kondakta anapoanza kuwa na utovu wa nidhamu
Maoni