Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba 14, 2018

Taifa Stars ya Amunike usipime, yafufua matumaini ya Cameroon

MATUMAINI YA KUENDA  CAMEROON YAFUFUKA CHEREKO! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kuichapa bila huruma Cape Verde kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa Afrika nchini Cameroon mwakani.  Stars inayonolewa na staa wa zamani wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Nigeria, Emmanuel Amunike imepata ushindi huo kufuatia magoli yaliyofungwa kila kipindi na mastaa wake wanaocheza soka la kimataifa, Simon Msuva anaecheza Morocco akifunga goli la kwanza huku Nahodha Mbwana Samatta 'Poppa' akifunga goli la pili.  Samatta ambaye anakipiga Genk ya Ubelgiji inayoshiriki pia michuano ya Europa angeweza kuipa Stars goli baada ya mkwaju wake aliopiga kugonga mwamba kabla ya dakika chache mbele kutengeneza goli la kuongoza lililofungwa na Msuva

Serikali yagomea wapelelezi wa nje kuchunguza sakata la MO Dewji

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema Serikali haiwezi kuruhusu vyombo vya ulinzi na usalama kutoka nje ya nchi kuchunguza tukio la kutekwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’.  Masauni ametoa kauli hiyo leo Jumanne Oktoba 16, 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari.  Amesema anaamini polisi kuna wataalamu wanaoijua kazi yao, wanaifanya kwa kuzingatia maadili.  “Kuna haja gani kuleta vyombo vya nje wakati tuna jeshi bora na lenye uelewa mkubwa licha ya kukabiliwa na changamoto za hapa na pale,” amesema.  Amesema  polisi hawajashindwa kuchunguza jambo hilo na lipo ndani ya uwezo wao.  Alipoulizwa kuhusu familia ya Mo Dewji kutangaza dau la Sh1bilioni kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazofanikisha kupatikana kwa mfanyabiashara huyo, Masuani amesema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa si msemaji wa familia. Hata hivyo, amesema wananchi wana nafasi ya kutoa taarifa kwa polisi  ili wawe...