Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya UMEME

Tanzania yatia saini ujenzi wa mradi wa umeme unaopigiwa kelele na wanamazingira, Rais Magufuli asema ni mradi wa lazima kwa maendeleo

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Tanzania John Magufuli amesema kutekelezwa kwa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme wa Stigler's Gorge ni jambo la lazima. Leo rais wa nchi hiyo John Magufuli ameweka saini na wakandarasi wa mradi huo kutoka Misri wakiwa pamoja na waziri mkuu wa nchi yao. Hatua hiyo inakuja baada ya miaka 40 tangu utafiti wa uzalishaji wa umeme kutoka mto Rufiji ambao unaweza kuzalisha megawati 2,100 kufanyika wakati huo Tanzania ikiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere. Mradi huu unatarajiwa kutekelezwa na fedha za watanzania wenyewe kwa kiwango cha dola za kimarekani bilioni 2.9 ambayo ni sawa na takribani shilingi trilion 6.5 za kitanzania. Na kampuni itakayofanya kazi hiyo inatoka Misri. Rais Magufuli amesema kwamba walitumia muda kutafakari kuhusu mradi huu kwa sababu Tanzania imebarikiwa na vyanzo vingi sana vya uzalishaji umeme kama vile maji,gesi asilia,upepo,joto ardhi ,makaa ya mawe pamoja na madini ya urani. Na kufikia uamuzi huo wal...