Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya KOMBE LA DUNIA

Luis Enrique kocha mpya wa Uhispania

Kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique ameteliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Uhispania Kocha  wa  zamani  wa  klabu  ya  Barcelona  Luis Enrique ametia saini mkataba  wa  miaka  miwili  kuchukua  hatamu za kuifunza  timu ya  taifa  ya  Uhispania. Anachukua  nafasi  ya  Julen lopetegui, ambaye  alifutwa  kazi katika  mkesha  wa  kuanza  kwa  fainali  za kombe  la  dunia  baada  ya  kukubali kazi katika  timu  ya  Real Madrid. Fernando Hierro alichukua  udhibiti wa  timu  hiyo  kwa  muda  kwa ajili  ya  fainali  hizo, ambapo  mabingwa  hao  wa  mwaka  2010 wa kombe  la  dunia  waliondolewa  katika  awamu  ya  mtoano na wenyeji Urusi

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 10.07.2018

Beki wa zamani wa Real Madrid Michel Salgado anaamini mshambuliaji wa Tottenham na Uingereza Harry Kane, 24, ndiye anayelengwa na klabu hiyo msimu huu baada ya mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 26. (Talksport) Chelsea inajaribu kuipiku Manchester City katika kumsaini kiungo wa kati wa Lazio na Itali Jorginho, 26. (Manchester Evening News) City pia imembishia hodi kiungo wa kati wa Real Madrid na Croatia Mateo Kovacic, 24, huku wakiwa na wasiwasi kuhusu kumtia mkobani Jorginho. (Mirror) Mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 29, anatarajiwa kusalia na klabu hiyo licha ya kuhusishwa na uhamisho (Bild) Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Roma Monchi anasema kuwa ataangazia maombi ya kumuuza kipa wa Brazil Alisson lakini kufikia sasa hakuna klabu iliowasilisha ombi la kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (FourFourTwo) Manchester United na Real Madrid wamekutana na maafisa kutoka Lazio kujadili uhamisho wa kiungo wa...

Misri watoa ripoti ya Salah kuhusu Kombe la Dunia

Baada ya jana Mohamed Salah kuumia kwenye mchezo wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Real Madrid na Liverpool, Daktari wa timu ya taifa ya Misri Dkt. Mohammed Abu Ola amesema nyota huyo ana nafasi kubwa ya kucheza Kombe la Dunia. Dkt. Abu Ola amesema baada ya mchezo aliwasiliana na daktari wa timu ya Liverpool na kumweleza kuwa picha za mionzi (X-ray) zimeonesha bega la Salah limeteguka kwenye mfupa mdogo na matibabu yalianza haraka ili aweze kupona kwa wakati. Kwa mujibu wa Dkt. Abu Ola na daktari wa Liverpool Salah atakuwepo kwenye fainali za Kombe la Dunia. Salah aliumizwa na mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos na kutolewa dakika ya 31 baada ya kushindwa kuendelea na mchezo ambapo timu hizo zilikuwa bado hazijafungana.  Baada ya Salah kutoka Real Madrid walifanikiwa kushinda kipindi cha pili kwa mabao 3-1 na kutwaa ubingwa wa 13 na wa taatu mfululizo chini ya kocha Zinedine Zidane ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo. Mabao ya Real Madrid yalifungwa ...