Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya LIBERIA

Rais mteule George Weah awataka raia wa Liberia walio nchi za kigeni kurudi nyumbani kuijenga nchi

Weah awataka raia wa Liberia walio nje kurudi kuijenga nchi Rais aliyechaguliwa nchini Liberia George Weah, amewashauri raia wa Liberia wanaoishi nchi za ng'ambo kurudi nyumbani ili kusaidia kuijenga nchi yao. Alitoa wito huo wakati wa mkutano wa kwanza na waandishi wa habari tangu atangazwe mshindi katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais. George Weah achaguliwa kuwa Rais wa Liberia Nyota huyo wa zamani wa kandanda alisema ujuzi wa watu wa Liberia walio nchi za kigeni unahitajika kuijenga nchi hiyo. Bw. Weah alipongezwa aliposema kuwa ufisadi hautavumiliwa katika utawala wake. Anaingia madarakani rasmi mwezi Januari.

George Weah achaguliwa kuwa Rais wa Liberia

MTEULE THE BEST George Weah Leo atangazwa kuwa Rais wa Liberia na tume ya uchaguzi nchini humo Mwanasoka maarufu George Weah ashinda urais Liberia George Weah Leo atatangazwa kuwa Rais wa Liberia na tume ya uchaguzi nchini humo baada ya kuongoza kwa asilimia 61.5 kati ya kura asilimia 98.1 zilizohesabiwa. Bwana Weah amemtangulia mpinzani wake Joseph Boakai kwa kura asilimia 60. Anachukua nafasi ya mwanamke wa kwanza Afrika kuwa rais Bi.Ellen Johnson Sirleaf anayemaliza muda wake kwa mujibu wa katiba ya taifa hilo na ambaye pia ni mshindi Nobel. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa nchi hio kupata kiongozi kwa njia ya kidemokrasia. baada ya matokeo kutangazwa. "Ninazielewa umuhimu na majukumu ya kazi kubwa niliyokabidhiwa leo. Mabadiliko yanakuja." George Weah ni nani? Weah ni mwanasoka maarufu aliyecheza kwenye klabu za soka za juu Ulaya kama Paris St-Germain (PSG) na AC Milan, kabla ya kumaliza taaluma yake nchini Uingereza kwa kuwachezea kwa muda mfupi klabu za Chelsea...

Leo ni duru ya pili ya uchaguzi wa rais Liberia kati ya George Weah na Joseph Boakai

Duru ya pili ya uchaguzi wa urais Liberia kati ya George Weah (kushoto) na Joseph Boakai Watu nchini Liberia wanapiga kura katika duru ya pili kati ya makamu wa rais Joseph Boakai na nyota wa zamani wa kandanda George Weah. Bwana Weah, 51, alishinda duru ya kwanza lakini hakufanikiwa kupata asilimia 50 ya kura kumwezesha kuwa mshindi. Duru ya pili ya uchaguzi wa urais kuchukua mahala pake Ellen Johnson Sirleaf, ilichelewa kufuatia kesi iliyokuwa mahakamani. Vituo vya kupigia kura vinafunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa kumi na mbili. Zaidi ya watu milioni mbili wamejiandikisha kama wapiga kura. Wagombea ni nani ? Bw. Boakai 73, amekuwa makamu wa rais nchini Liberia kwa miaka 12 lakini haonekani kunufaika na uungwaji mkono kutoka kwa rais. Naye Weah, ambaye ni nyota wa zamani wa kandanda ana matumaini ya kushinnda baada ya kuwania kwa mara ya tatu. Alimshinda Bi Johnson Sirleaf wakati wa duru ya kwanza mwaka 2005, lakini akashindwa wakati wa duru ya pili. Wakati wa ...