Mhe.Mchengerwa ataka kukamilika kwa ujenzi wa barabara jimbo la Ukonga kwa wakati.
Mhe.Mchengerwa ataka kukamilika kwa ujenzi wa barabara jimbo la Ukonga kwa wakati. Na John Mapepele Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Mohamed Mchengerwa amemtaka mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Barabara ya Banana – Kitunda – Kivule – Msongola na Kivule – Majohe Junction, barabara za Kiwalani na Migombani kukamilika mradi huo kwa wakati bila kutoa visingizio vyovyote kwa kuwa tayari Serikali imeshamlipa fedha zote. Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo jana wakati akikagua mradi huo akiambatana na Mbunge wa jimbo la Ukonga Mhe. Jerry Silaa. Amesema dhamira ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kuwa miundombinu ya barabara zote nchini inakamilika ili ziweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka. Aidha, amefafanua kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara utasaidia kuboresha maisha ya wananchi kwa kuwa shughuli za uchumi zitaimarika . Amempongeza Mhe. Rais kwa kutoa fedha nyingi kutengeneza miradi mbalimbali ya barabara hapa nchini huku ...