Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya RUSHWA YA NGONO

Mwalimu kuburuzwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa

Mwalimu kuburuzwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa Taassis ya kuzuaia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mtwara inatarajia kumfikisha Mahakamani aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Masasi, Mwanaid Abdalah Mtaka kwa tuhuma za kutumia nyaraka za uongo na kujipatia fedha kiasi cha Shilingi 1,578,000. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Takukuru Mkoani humo, Stephen Mafipa , amesema kuwa Mtaka anakabiliwa na kosa la jinai kwa kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajiri wake kisha kujipatia kiasi hicho cha fedha jambo ambalo ni kinyume na sheria. “Alitumia na kuwasilisha stakabadhi zenye kuonyesha alitumia jumla ya shilingi 1,578,000/= kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya shule ya Msingi Masasi, hukub akijua kwamba hakununua,”Amesema Mafipa. Aidha, kitendo hicho kilimuwezesha mtuhumiwa kujipatia kiasi cha shilingi 1,578,000/= ambazo alizitumia kwa matumizi yake binafsi. Kesi hiyo ya Jinai itafunguliwa katika mahakama ya wilaya...

Vicensia Shule: Aliyekuwa na ujumbe wa Magufuli aitwa kamati ya maadili

Dkt Vicensia Shule anasema ulinzi wa Dkt Magufuli ulimfanya anyamae Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) aliyezua mjadala mtandaoni baada ya kudai kwamba rushwa ya ngono imekithiri chuoni humo ameitwa kufika kwenye kamati ya maadili ya chuo hicho. Barua ya kamati hiyo iliyotiwa saini ya mwenyekiti Prof Evelyne Mbede inamtaka mhadhiri huyo kufika mbele ya kamati hiso Ijumaa saa tisa "ili kamati iweze kulifanyia kazi swala hili kwa haraka." Dkt Vicensia Shule alikuwa ameandika kwenye Twitter kwamba alitaka sana kuufikisha ujumbe wake kwa Rais John Magufuli lakini aliwaogopa walinzi wake. Dkt Magufuli alikuwa amezuru chuo hicho kufungua maktaba mpya, kubwa na ya kisasa ya Kikuu cha Dar es Salaam iliyojengwa katika Kampasi Mlimani (Mwalimu. Julius K. Nyerere) jijini Dar es Salaam. Maktaba hiyo kubwa Afrika Mashariki na Kati ilijengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 93.6 ikiwa ni msaada kutoka Serikali ya China na ndiyo maktaba kubwa kuliko maktaba zote ambazo Ch...