Natii wito wa Ndugai, nataka kujua mambo ya hovyo hovyo nayoyafanya- Masele Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM) na Makamu wa kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika (Pan- African Parliament – PAP), Steven Masele amesema kuwa ameamua kuitikia wito wa Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ili kuweza kujua ni mambo gani ya hovyo hovyo anayoyafanya. Ameyasema hayo wakati akizungumza na DW ambapo amedai kuwa yeye alikuwa akitimiza majukumu yake ya kuongoza kamati maalum ya uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili rais wa bunge la Afrika, Nkodo Dang. Amesema kuwa anarejea nyumbani Tanzania ili kuitikia wito huo na kutaka yawekwe wazi kwa wananchi hayo mambo ya hovyo hovyo anayoyafanya huko Afrika Kusini sehemu ambayo ni kituo chake cha kazi. ”Nimemsikiliza Spika wangu Job Ndugai sijamuelewa, niko njiani narudi nyumbani Tanzania kuweza kujua hayo mabo ya hovyo hovyo ninayoyafanya ni yapi, na pale nilikuwa natekeleza majuk...