Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Masele: Natii wito wa Ndugai, nataka kujua mambo ya hovyo hovyo nayoyafanya







Natii wito wa Ndugai, nataka kujua mambo ya hovyo hovyo nayoyafanya- Masele

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM) na Makamu wa kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika (Pan- African Parliament ā€“ PAP), Steven Masele amesema kuwa ameamua kuitikia wito wa Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ili kuweza kujua ni mambo gani ya hovyo hovyo anayoyafanya.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na DW ambapo amedai kuwa yeye alikuwa akitimiza majukumu yake ya kuongoza kamati maalum ya uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili rais wa bunge la Afrika, Nkodo Dang.

Amesema kuwa anarejea nyumbani Tanzania ili kuitikia wito huo na kutaka yawekwe wazi kwa wananchi hayo mambo ya hovyo hovyo anayoyafanya huko Afrika Kusini sehemu ambayo ni kituo chake cha kazi.

ā€Nimemsikiliza Spika wangu Job Ndugai sijamuelewa, niko njiani narudi nyumbani Tanzania kuweza kujua hayo mabo ya hovyo hovyo ninayoyafanya ni yapi, na pale nilikuwa natekeleza majukumu yangu,ā€amesema Masele

Aidha, ameongeza kuwa kamati iliyokuwa ikimchunguza rais wa bunge la Afrika imetoa ripoti yake kuwa rais huyo amekutwa na tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi, ikiwemo undugu, rushwa na unyanyasaji wa kingono kwa watumishi kike.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kwasasa yeye ndiye anaye kaimu kiti hicho kipindi ambacho rais wake akichunguzwa kwa undani zaidi kuhusu tuhuma zinazomkabili za matumizi mabaya ya ofisi na unyanyasaji wa kingono

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...