Alikiba na AY wakiwa na wake zao
Wasanii kama Alikiba, Ben Pol na AY, wote wamefanikiwa kuoa nje ya nchi, huku Ben Pol akiwa mbioni kumuoa mpenzi wake Anerlisa ambaye ni raia wa Kenya baada ya kumvisha pete ya uchumba hivi karibuni. Alikiba pia ameoa Kenya na AY amemuoa mrembo raia wa Rwanda.
Mwijaku ambaye ni muigizaji maarufu nchini na mtu maarufu katika mitandao ya kijamii, amezitaja sababu 5 zinazopelekea wasanii wa Tanzania kuamua kuoa nje ya nchi.
Sababu ya kwanza ameitaja kuwa ni uoga wa wasanii wa kiume maarufu Tanzania, kutokana kuwa wanahisi wanawake wa Kitanzania wanawafahamu nje ndani.
Sababu ya pili ni kuogopa kuchaguliwa au kukosolewa uchaguzi wa wanawake wao na ndugu wa familia. Mtazame hapa chini Mwijaku akielezea zaidi sababu hizo
Maoni