Mkutano wa Makardinali wa 11 ulifanyika na kiapo kwa wasaidizi wa mkutano mkuu

KILINGENI walitoa kiapo cha usiri kabisa. (ANSA) Conclave: maofisa na wahusika wengine walitoa kiapo cha usiri kabisa. (ANSA) Mkutano wa 11 wa Makardinali ulifanyika jioni na mijadala kama 20 hivi ilihusiana na mada kubwa ya umuhimu wa kichungaji na kikanisa.Na wale watakaosaidia katika mkutano wa uchaguzi walitoa kiapo cha usiri kabisa kwa mujibu wa katiba ya Kitume ya Universi Dominici Gregis.Miongoni mwao mshehereshaji wa liturujia za kipapa,watu wa sakrestia,usafi,madaktari,manesi na waungamishi. Vatican News Mkutano wa 11 wa makardinali ulifanyika saa kumi na moja jioni kwa kufunguliwa na sala ya pamoja. Walikuwapo makardinali 170, miongini mwake makardinali 132 wa kupiga kura. Mijadala kama 20 hivi ilijihusiana na mada kubwa ya umuhimu wa kichungaji na kikanisa. Muda ulitolewa kwa suala la ukabila ndani ya Kanisa na katika jamii. Uhamiaji ulijadiliwa, kwa kutambua wahamiaji kama zawadi kwa Kanisa, lakini pia kusisitiza uharaka wa kusindikizana nao na kuunga...