Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MWANAMKE

​Anna Kikina amerudi nyumbani! Ilikuwa imepita miaka minane tangu mwanamke wa Urusi aende angani.

Anna Kikina aliondoa pengo hilo la muda mrefu aliporuka hadi Kituo cha Kimataifa cha Anga kwa kutumia chombo cha anga za juu cha Elon Musk's Crew Dragon, kama sehemu ya misheni ya Crew-5.  Alitumia siku 157 huko, na aliingia tena kwenye mzunguko mnamo Machi 12, juu ya Ghuba ya Mexico. Baada ya kupitia ukarabati katika Kituo cha Nafasi cha Houston, Anna alisafiri kwenda Moscow.  Kwa njia, Kikina kwa sasa ndiye mwanaanga wa kike wa Kirusi pekee. Kinachovutia sana ni kwamba aliwahi kuwa DJ wa kawaida wa redio katika eneo lake la asili la Siberia, kabla ya kugundua kuwa yeye pia anaweza kuwa mwanaanga.  Barabara ilikuwa ndefu: takriban miaka 10 ilikuwa imepita tangu kuanza kwa mafunzo yake ya kimsingi hadi safari yake ya anga.  Lakini tunafurahi sana kwamba alitimiza ndoto yake!

Serikali kujenga mabweni wanafunzi wasipate mimba

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mwita Waitara amesema mpango wa Serikali ni kujenga Mabweni katika Shule zote za Msingi na Sekondari, ili kuwanusuru na wanafunzi wa kike na suala la mimba. Mwanafunzi mwenye mimba Naibu Waziri Waitara ametoa kauli hiyo, wakati akizungumza Bungeni jijini Dodoma leo Novemba 15, 2019 wakati wa kipindi cha maswali na majibu kutoka kwa Wabunge kwenda kwa Mawaziri. Waitara amesema kuwa " mpango wa Serikali ni kujenga Mabweni katika Shule zote za Msingi na Sekondari ili watoto wakike wapate sehemu za kukaa na tuwaepushe na mimba zitakazowafanya washindwe kuendelea na masomo ." Leo Novemba 15, 2019 Bunge hilo linatarajiwa kuahirishwa baada ya kujadili mpango wa maendeleo ya Taifa kwa mwaka ujao wa fedha. Serikali kujenga mabweni ili wanafunzi wasipate mimba.

Mtoto wa siku mbili atupwa kandokando ya ziwa Victoria

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limefanikiwa kumuokota mtoto mmoja wa kike akiwa hai anayekadiriwa kuwa na umri wa siku 2 hadi 3 baada ya kutupwa kichakani kandokando mwa ziwa Victoria na mtu asiyefahamika maeneo ya Bwiru ziwani Wilayani Ilemela.  Tukio hilo limetokea Novemba 1, 2018  hii ni baada ya watu waliokua wakipita njiani kusikia sauti ya mtoto akilia toka kichakani ndipo walifuatilia na walipoona ni mtoto walitoa taatifa Polisi.  Polisi walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kukuta mtoto wa kike akiwa ametupwa kichakani hapo akiwa hai huku mwili wake ukiwa umeviringishwa kwenye mfuko wa sandarusi.  Jeshi la Polisi limeeleza kuwa Mtoto huyo amepata matibabu na hali yake inaendelea vizuri amekabidhiwa katika shirika la Forever Angel lililopo Bwiru Wilayani  Ilemela kwa ajili ya hifadhi.  Hata hivyo Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi pamoja na msako mkali wa kumtafuta mama wa mtoto huyo

Kuna changamoto na athari kubwa sana ukioa mwanamke mzuri

AWALI ya yote naomba niseme kwamba, raha ya ndoa ni kumpata mtu ambaye anajua maisha na anajua mapenzi pia. Ukipata mwanamke ambaye anajua kutafuta pesa tu lakini kwenye ulimwengu wa mapenzi ni limbukeni, atakusumbua sana.  Lakini pia ukijichanganya ukaoa mwanamke ambaye ni mtaalam wa mapenzi lakini hajui pesa inavyotafutwa, nalo ni tatizo licha ya kwamba kwa wengine si tatizo kwani wapo ambao hawataki kuoa wanawake wenye vipato kutokana na yale yanayosemwa kuwa, baadhi yao wakijua kutafuta pesa, wanakuwa viburi.  Hata hivyo, kwa wanaume wanapofikia muda wa kuoa kila mmoja huwa na chaguo lake. Kila mtu atakuwa na vigezo vyake ambavyo vinaweza kutofautiana kutoka kwa mmoja hadi kwa mwingine.  Tofauti hiyo inakuja hata kwenye suala la tabia na uzuri. Kwa mfano, wapo ambao wanaangalia sana suala la tabia nzuri na muonekano mzuri pia. Lakini unaweza kushangaa mwanaume akatafuta mwanamke ambaye anakunywa pombe na anayependa kujirusha kwa kuwa na yeye ni mtu wa mamb...