Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya NEMC

Ofisi ya Makamu wa Rais imesema mchakato wa kulipa mamlaka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)

Picha
Mhe. Khamis Hamza Khamis Ofisi ya Makamu wa Rais imesema mchakato wa kulipa mamlaka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji kupitia mchakato unaoendelea. Kuifanya NEMC kuwa mamlaka kutaipa nguvu ya kisheria ya kusimamia majukumu yake ipasavyo na hivyo kujiwezesha kimapato. Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ameliarifu Bunge jijini Dodoma leo tarehe 12 Mei, 2025 wakati akijibu swali la nyongeza Mbunge wa Mpendae Mhe. Toufiq Salim Turky lililoulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Viti maalumu Mhe. Amina Ali Mzee aliyetaka kujua ni lini mchakato wa NEMC kuwa mamlaka kamili. Mhe. Khamis amesema Mchakato wa kulifanya Baraza hilo kuwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira (NEMA) tayari umekwishaanza na pindi utakapokamilika utawasilishwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na kutolewa maamuzi. Alifafanua kuwa changamoto inayosababisha kuchelewa kwa vyeti vya tathmini ya athari kwa mazing...