Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya FIFA AWARD

Misri watoa ripoti ya Salah kuhusu Kombe la Dunia

Baada ya jana Mohamed Salah kuumia kwenye mchezo wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Real Madrid na Liverpool, Daktari wa timu ya taifa ya Misri Dkt. Mohammed Abu Ola amesema nyota huyo ana nafasi kubwa ya kucheza Kombe la Dunia. Dkt. Abu Ola amesema baada ya mchezo aliwasiliana na daktari wa timu ya Liverpool na kumweleza kuwa picha za mionzi (X-ray) zimeonesha bega la Salah limeteguka kwenye mfupa mdogo na matibabu yalianza haraka ili aweze kupona kwa wakati. Kwa mujibu wa Dkt. Abu Ola na daktari wa Liverpool Salah atakuwepo kwenye fainali za Kombe la Dunia. Salah aliumizwa na mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos na kutolewa dakika ya 31 baada ya kushindwa kuendelea na mchezo ambapo timu hizo zilikuwa bado hazijafungana.  Baada ya Salah kutoka Real Madrid walifanikiwa kushinda kipindi cha pili kwa mabao 3-1 na kutwaa ubingwa wa 13 na wa taatu mfululizo chini ya kocha Zinedine Zidane ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo. Mabao ya Real Madrid yalifungwa ...

FIFA waikataa rekodi ya Romelu Lukaku na kupunguza mabao yake.*

Mashabiki wa Ubelgiji na Manchester United jana walijawa na furaha baada ya kusikia kwamba mshambuliaji wao Romelu Lukaku amevunja rekodi ya ufungaji katika timu yao ya taifa. Romelu Lukaku alitajwa kuvunja rekodi hiyo kwa kuwapita Bernard Voorhoof na Paul Van Himst ambao wana mabao 30 huku goli dhidi ya Japan likimfanya yeye kufikisha 31 idadi ambayo hata Lukaku mwenyewe alijinasibu kuifikia. Lakini sasa shirikisho la soka duniani FIFA limeibuka na kutoitambua rekodi hiyo ya Romelu Lukaku kwa kusema kwamba moja kati ya michezo ambayo Lukaku alifunga hautambuliki na shirikisho hilo. Mechi hiyo ilikuwa mwaka 2014 ambapo Ubelgiji walicheza dhidi ya timu ya taifa ya Luxembourg ambapo Ubelgiji waliibuka kidedea kwa mabao 5 huku Romelu Lukaku akifunga mabao 3 kati ya hayo 5. Kinachowafanya FIFA kuundoa mchezo huo kwenye rekodi zao ni kitendo cha Ubelgiji kufanya sub 7 badala ya 6 katika mchezo huo suala ambalo lilikuwa kinyume na sheria katika mechi hiyo. Hii sasa inamaanisha Lukaku a...

Cristiano Ronaldo ● FIFA THE BEST PLAYER 2017_HD video and photo

Hatua zilizo mfanya CR7 Kushinda tuzo MTEULE THE BEST CRISTIANO RONALDO KIKOSI BORA CHA DUNIA 2017/2018 CR7 JR akimsalimia Messi CR7 Fans