Wakaazi wa kijiji cha Nakapyata, wilayani Buyende nchini Uganda wamefanya sherehe ambapo watoto wawili walio kati ya umri wa miaka tisa na sita waliozwa katika utamaduni wa kushangaza. Kulingana na mtandao wa gazeti la Daily Monito r nchini Uganda Uganda, mvulana huyo ambaye yuko katika darasa la nne katika shule ya msingi ya Buyende na msichana ambao wote waliripotiwa kuzaliwa na meno mawili waliozwa siku ya Jumatatu na kupatiwa nyumba ya kitamaduni kuishi. Chini ya sheria za Uganda , ni makosa kwa watu walio chini ya umri wa miaka 18 kufunga ndoa ama hata kushiriki katika tendo la ngono. Inadaiwa kuwa watoto hao wawili walianza kuchumbiana wakati mvuana alipokua na miaka mitatu na msichana akiwa na umri wa miezi mitatu pekee. Hatua hiyo baadaye iliimarisha uhusiano kati ya familia zote mbili , huku Delifazi Mulame babake mvulana akimuita msichana huyo kama 'mke wa mwanangu'. ''Mwanangu alizaliwa na meno mawili na mkewe akazaliwa na meno mawili. Kuzaliwa kwak...