WAZIRI MKUU WA TANZANIA AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA BELARUS
Washuhudia utiaji saini hati tatu za makubaliano na mkataba mmoja WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na Waziri Mkuu wa Belarus, Alexander Turchin na kujadiliana naye masuala ya uwekezaji, biashara, nishati, madini, elimu, afya, teknolojia na kilimo kwenye kikao kilichofanyika leo (Jumanne, Julai 22, 2025) ofisini kwa mwenyeji wake, mtaa wa Sovetskaya, jijini Minsk. Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu Majaliwa alimweleza mwenyeji wake kuwa, mbali na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia anataraji kuwa ziara hiyo itaongeza chachu ya nchi hiyo kushirikiana na Tanzania kwenye masuala mbalimbali ikiwemo uwekezaji, elimu, afya na upatikanaji wa zana za kisasa kwenye kilimo kutokana na fursa mbalimbali zilizoko nchini. Alisema mazungumzo yao yamefungua milango ya kuimarisha uwekezaji, fursa za biashara na masomo katika vyuo vya elimu ya juu, na kwamba wamekubaliana na mwenyeji wake kuwa Mawaziri wake na Naibu Makatibu Wakuu walioko kwenye ziara hiyo wakutane ili kuanza ...