Serikali ya Marekani iliahidi kutoa dola milioni 1 kwa ajili ya yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kutambua ni wapi alipo Mwana wa kiume wa muasisi wa al-Qaeda Osama Bin Laden, Hamza,amefariki , kwa mujibu wa maafisa wa ujasusi wa Marekani. Taarifa kuhusu mahala au tarehe ya kifo cha Hamza Bin Laden bado haijawa wazi katika ripoti ya chanzo hicho cha habari. Mwezi Februari, Serikali ya Marekani iliahidi kutoa dola milioni 1 kwa ajili ya yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kutambua ni wapi alipo. Hamza Bin Laden, anayedhaniwa kuwa na umri wa miaka 30, alikuwa ametoa ujumbe mbalimbali wa sauti na video akitoa wito wa kufanya mashambulio dhidi ya Marekani na nchi nyingine. Ripoti zilitolewa kwanza na mashirika ya habari ya NBC na New York Times. Hamza Bin Laden aliwatolea wito wapiganaji wa jihadi kulipiza kisasi mauaji ya baba yake aliyeuliwa na kikosi maalum cha Marekani nchini Pakistan mnamo mwezi Mei 2011. Kadhalika alikuwa amewatolea wito watu wa rasi ya A...