Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Hamza Bin Laden: Mwana wa kiume wa Osama 'amefariki', yasema Marekani





Serikali ya Marekani iliahidi kutoa dola milioni 1 kwa ajili ya yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kutambua ni wapi alipo

Mwana wa kiume wa muasisi wa al-Qaeda Osama Bin Laden, Hamza,amefariki , kwa mujibu wa maafisa wa ujasusi wa Marekani.

Taarifa kuhusu mahala au tarehe ya kifo cha Hamza Bin Laden bado haijawa wazi katika ripoti ya chanzo hicho cha habari.

Mwezi Februari, Serikali ya Marekani iliahidi kutoa dola milioni 1 kwa ajili ya yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kutambua ni wapi alipo.

Hamza Bin Laden, anayedhaniwa kuwa na umri wa miaka 30, alikuwa ametoa ujumbe mbalimbali wa sauti na video akitoa wito wa kufanya mashambulio dhidi ya Marekani na nchi nyingine.



Ripoti zilitolewa kwanza na mashirika ya habari ya NBC na New York Times.

Hamza Bin Laden aliwatolea wito wapiganaji wa jihadi kulipiza kisasi mauaji ya baba yake aliyeuliwa na kikosi maalum cha Marekani nchini Pakistan mnamo mwezi Mei 2011.

Kadhalika alikuwa amewatolea wito watu wa rasi ya Arabia kulipiza kisasi. Saudi Arabia ilimyang'anya uraia mwezi Machi.

Aliaminika kuwa katika kifungo cha nyumbani nchini Iran lakini ripoti nyingine zilisema kuwa huenda alikuwa akiishi katika mataifa ya Afghanistan, Pakistan na Syria.



Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema kuwa nyaraka zilizokamatwa katika uvamizi wa mwaka 2011 katika nyumba ya baba yake ya Abbottabad, Pakistan, zinaonyesha kuwa Hamza Bin Laden alikuwa anaandaliwa kuchukua utawala wa al-Qaeda.

Vikosi vya Marekani pia viliripotiwa kubaini video hii ya harusi yake akimuoa binti wa afisa mwingine wa ngazi ya juu wa al-Qaeda ambayo ilidhaniwa kufanyika nchini Iran:

Baba mkwe wake alikuwa ni Abdullah Ahmed Abdullah au Abu Muhammad al-Masri, ambaye anatafutwa kwa madai ya kuhusika katika mashambulio ya ugaidi ya mwaka 1998 dhidi ya balozi za Tanzania na Kenya.

Al-Qaeda lilikuwa ni kundi lililotekeleza mashambulio mabaya ya ugaidi ya Septemba 11, 2001 dhidi ya Marekani, lakini hadhi yake kwa sasa imeshuka katika kipindi cha miongo kadhaa iliyopita baada ya kuibuka kwa umaarufu wa kundi la Islamic State.

Alikuzwa katika misingi ya kuichukia Marekani

Ni ishara ya jinsi taarifa chache kumuhusu Hamza Bin Laden kiasi kwamba maafisa hawakuweza kuthibitisha umri wake.

Katika miezi ya hivi karibuni walisema kuwa huenda alikuwa nchini Afghanistan, Pakistan au Iran. lakini hawakuweza hata kusema ukweli hasa ni nchi gani mmoja wa watu ambao Marekani ''inawatafuta sana'' anaishi.

Zawadi ya dola milioni moja kwa yeyote atakayetoa taarifa kumuhusu ilikuwa ni hatua si tu ya uwezekano wa hatari anayoweza kusababisha lakini pia ilikuwa ni ishara ya umuhimu kwa al-Qaeda na propaganda yao.



Hamza alikuwa ni mtoto pekee aliyekuwepo wakati baba yake aliposaidia kupanga njama za mashambulio ya Septemba 11 lakini, kwa mujibu wa wakuu wa kundi hilo lenye itikadi kali, alikuwa pamoja naye wakati wa mashambulio hayo.

Kwa mtoto wa kiume ambaye alikuwa akifundishwa kuichukia Marekani, kukwepa mauaji ya ulipizaji kisasi mikononi mwa kikosi maalumu lingekuwa ni jambo ambalo lingesalia akilini mwa watu.

Katika miaka ya hivi karibuni alituma ujumbe mtandaoni akitoa wito kwa mashambulio dhidi ya Marekani na washirika wake.

Al-Qaeda: Taarifa muhimu


Osama Bin Laden akiwa karibu na Kabul mwaka 2001

Alifahamika nchini Afghanistan katika miaka ya mwisho ya 1980, kama mwarabu aliyejitolea kujiunga na kikosi cha Afghanstan kilichoungwa mkono na mujahideen kilichopigana kuvifukuza vikosi vilivyoteka eneo la Usovieti


Osama Bin Laden alianzisha shirika la kusaidia wahudumu wa kujitolea ambalo lilikuja kutambuliwa kama al-Qaeda, au "ngome"


Aliondoka Afghanistan mnamo mwaka 1989, na kurejea tena mwaka 1996 kuongoza makambi ya mafunzo ya kijeshi ya maelfu ya waislamu kutoka mataifa ya kigeni.


Al-Qaeda ilitangaza "vita vitakatifu " dhidi ya Wamarekani,wayahudi na washirika wao


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...