Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Je Uchina na Urusi zitasaini mkataba mpya wa nyuklia?













Urusi inakana kuunda silaha zinazokiuka mkataba huo

Rais wa Marekani Donald Trump amesema anataka mkataba mpya wa nyuklia usainiwe na Russia na China kwa pamoja.

Bwana Trump amesema amekuwa akizungumza na na nchi hizo mbili kuhusu wazo hilo na wote "walilifurahia sana sana".

Kauli zake Trump zinakuja baada ya Marekani kujiondoa kwenye mkataba muhimu wa nyuklia na urusi , ikielezea juu ya aina mpya ya silaha.

Enzi ya Vita Baridi mkataba wa zana za masafa ya katikati (INF) ulisainiwa na rais wa Marekani Ronald Reagan na kiongozi wa iliyokuwa Sovieti Mikhail Gorbachev mnamo 1987. Mkataba huo (INF) ulipiga matrufuku matumizi ya zana za masafa ya kati yanayopiga kilomita 500 hadi 5,500 (310-3,400 miles).

Kujiondoa kwa Marekani kwenye mkataba huo Ijumaa kumefuatia shutuma za marekani kwamba Urusi ilikuwa imekiuka mkaataba huo kwa kuunda mtambo mpya wa mfumo makombora . Moscow imekanusha haya.



Akijibu maswali juu ya ni vipi ataepuka silaha za nyuklia kufuatia kuvunjika kwa mkataba wa INF , Bwana Trump amesema utawala wake umekuwa ukizungumza na Urusi Russia "kuhusu mkataba wa nyuklia, ili waachane na baadhi ya silaha, waachane na baadhi ".

"Tutahitaji kwa vyovyote vile kuijumuisha Uchina wakati fulani ,"aliongeza.

Bwana Trump amesema mkataba wa aina hiyo unaweza kuwa "kitu cha kizuri kwa dunia " na kwamba anaamini hili litatekelezwa.

"Uchina ilifurahia sana, sana kuhusu kuzungumzia juu ya suala hili na ilikuwa hivyo hivyo kwa Urusi . Kwa hiyo ninadhani tutakuwa na mkataba wakati fulani ", Trump aliwambia waandishi wa habari

Ni kwanini Trump alijiondoa kwenye mkataba ?

Marekani zimeishutumu Urusi kukiuka mkataba kwa kumiliki aina mpya ya silaha, kwa kutengeneza makombora kadhaa ya 9M729 - yanayofahamiwa na Nato kama SSC-8. Shutuma hizi pia ziliwasilishwa kwa washirika wa Marekani katika muungano wa Nato, ambao wote waliunga mkono madai ya Marekani.

"Urusi inawajibika kwa kuvunjika kwa mkataba'', amesema waziri wa mambo ya nje wa marekani Mike Pompeo katika taarifa aliyoitoa Ijumaa.

"Kwa uungaji mkono kamili wa washirika wetu wa Nato, Marekani imeamua kuwa Urusi ndio imesababisha kuvunja mkataba, imekuwa ikikiuka mara kwa mara wajibu wake chini ya mkataba ,"aliongeza.

---------------


Makombora mapya ya 9M729 ya Urusi yanaitia tumbo joto Marekani na washirika wake

Nato imesema inajiweka kando na mvutano kuhusu silaha mpya na Urusi, Katibu Mkuu wake ameeleza, baada ya Marekani kujiondoa rasmi kutoka kwenye mkataba wa nyukilia na Urusi.

Rais Donald Trump mnamo Februari ametangaza kuwa Marekani itajitoa kutoka mkataba huo iwapo Urusi haitotii, na kuweka tarehe ya mwisho kuwa Agosti 2.

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesitisha majukumu ya taifa lake katika mkataba huo muda mfupi baadaye.

Kuna hatari gani?

"Breki ya thamani katika vita vya nyuklia" inaeleka kupotea, ameonya katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres.





"Huenda hili likaongeza na sio kupungua tishio la makombora," aliongeza, na kuomba pande zote kutafuta "makubaliano mapya ya mtazamao wa pamoja ya udhibiti wa silaha kimatiafa".

Wachambuzi wanahofia kwamba kutibuka kwa makubaliano hayo ya kihistoria huenda kukachangia ushindani mpya wa silaha kati ya Marekani, Urusi na China.

"Kutokana na kuvunjika kwa mkataba huo sasa, tutashuhudia utengenezaji na utumiaji wa silaha mpya," Pavel Felgenhauer, mchambuzi wa zana za Urusi ameliambia shirika la habari la AFP. "Urusi tayari ipo tayari."

Mwezi uliopita, Katibu mkuu wa Nato Jens Stoltenberg ameiambia BBC kuwa makombora ya Urusi - ambayo alisema kuwa ni "ukiukaji wa wazi wa mkataba huo" - zina uwezo wa nyuklia, ambayo ni magumu kutamabua na yanaweza kufika katika miji ya Ulaya katika muda wa dakika.

Mkuu wa ujasusi Marekani ajitenga na utawala wa Trump.

Uturuki yaikaidi Marekani kwa kujihami na makombora ya Urusi.





"Hili ni jambo zito," aliongeza. " Mkataba wa INF umekuwa jiwe la msingi katika udhibiti wa silaha kwa miongo kadhaa, na sasa tunashuhudia kuvunjika kwa mkataba huo ."

Ameongeza kwamba hakujakuwepo "ishara zozote" kuwa Urusi itatii na makubaliano hayo na kwamba "ni lazima tujitayarishe kwa ulimwengu usiokuwa na mkataba wa INF na ulio na makombora zaidi ya Urusi".

Stoltenberg pia alisema kuwa uamuzi wowote wa Nato kuhusu namna gani ya kujibu utatolewa baada ya kupita muda huo wa mwisho uliotolewa.


Aina mpya ya makombora ya nyuklia inayodaiwa na Marekani kuuundwa na Urusi

nato haina mpango wa kutuma makombora yake ya ardhini Ulaya lakini makombora ya angani na ya ulinzi, ya mazoezi na utayari wa vikosi vyake na mipango mipya ya udhibiti wa silaha huenda yakawa ni sehemu ya jibu lake.

Mkataba wa (INF) ni nini?

Ulisainiwa na Marekani na uliokuwa Muungano wa Sovieti mnami 1987, mkataba huo ulipiga marufuku silaha zote za nyuklia na makombora yasio ya nyuklia ya masefu marefu na ya wastani isipokuwa ya baharini.

'



Marekani ilikuwa na wasiwasi kuhusu kutumwa kwa kombora la SS-20 la Sovieti mnamo 1979 na ilijibu kwa kuweka makombora ya masafa mafupi ya ardhini Ulaya - hatua iliyozusha maandamano makubwa.

Kufikia 1991, takriban makombora 2,700 yaliharibiwa.

Mataifa hayo mawili yaliruhusiwa kukagua hifadhi za taifa mwenza.

Mambo yaliharibika wapi?

Mnamo 2007, rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza kuwa mkataba huo haushughulikii maslahi ya Urusi.

Hilo lilifanyika baada ya rais wa Marekani George W Bush, mnamo 2002, kuitoa Marekani katika mkataba wa kupinga makombora ya masafa ya juu, uliopiga marufuku silaha zilizoundwa kuzuia makombora ya aina hiyo.





Mnamo 2014, rais wa wakati huo Marekani Barack Obama aliishtumu Urusi kwa kukiuka mkataba huo wa INF baada ya kutuhumiwa kufanya majaribio ya kombora la ardhini


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...