Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya SHERI ZA MPIRA WA MIGUU

David Beckham azungumza kiswahili

Aliyekuwa mchezaji wa kandanda wa timu ya taifa ya Uingereza David Beckham hajulikana kuwa na ujuzi wa kujua lugha nyingi lakini anaongoza kampeni dhidi ya malaria ambapo anaonekana akizungumza lugha tisa. Anaonekana katika filamu fupi akizungumzia vita dhidi ya Malaria na kupitia kamera na teknolojia ya tarakilishi anazungumza kiswahili, Kinyarwanda, Kiarabu, na kiarabu miongoni mwa lugha nyengine. Mdomo wake na uso unalingana na matamshi yake lakini sauti zinazosikika zinatoka kwa manusura wa ugonjwa wa malaria. Waandalizi wanatumai kwamba watu wengine duniani wataingia na kuongeza sauti zao. Sauti zitakazopatikana zitatumika kuwashinikiza viongozi duniani huku wakiandaa kufanya maamuzi kuhusu hazina ya kukabiliana na Ukimwi, TB na Malaria.

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

SHERIA 17 ZA SOKA ======================= Mchezo wa soka ni moja ya michezo maarufu sana duniani na ni biashara kubwa sana katika ulimwengu wa michezo na ukitaka kuamini hili angalia makampuni yaliyowekeza katika kudhamini soka – ni makampuni makubwa makubwa yenye hadhi ya kitaifa na kimataifa. Kwa kuzingatia aina hii ya wadhamini, waendeshaji wa mchezo wa soka, wameweka kanuni na miongozo ya kufuatwa ili kuhakikisha kuwa wale wanaowekeza pesa zao wanaona thamani ya uwekezaji wao. Kwa hiyo soka kama ilivyo katika michezo mingine inazo kanuni na tutajadili kanuni moja baada ya nyingine kama zilivobainishwa katika muongozo wa FIFA unaojulikana kwa jina la Law of the Game. Sheria Namba 1: Dimba ============== NYASI - Dimba la soka litakuwa la nyasi asilia au bandia kulingana na kanuni za masindano na nyasi hizo lazima ziwe za rangi ya kijani. Kwa dimba la nyasi bandia na kama mchezo unaochezwa utakuwa wa kutambuliwa na FIFA, basi nyasi hizo bandia lazima zikidhi viwango maalumu ...