Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya UKOLONI

Shujaa aliyewaongoza kupinga utawala wa kikoloni Afrika

Chifu Mkwawa: Shujaa aliyewaongoza Wahehe kupinga utawala wa kikoloni Afrika mashariki Fuvu la Chifu Mkwawa limewekwa ndani ya sanduku la kigae katika jumba la ukumbusho la Mkwawa huko Kalenga, Tanzania ya kati. Lakini kama taji, awali lilitundikwa katika nyumba ya afisa wa kikoloni huko Bagamoyo, kabla ya kuondolewa na kupelekwa Ujerumani - mkoloni wa mji huo - mwanzo mwa karne ya 20. Fuvu hilo lilitumika kuwatishia Wahehe, ambao waliongozwa na shujaa huyo katika vita vya kupinga utawala wa kikoloni wa Ujerumani. Na ufanisi wake ulikuwa ni mkubwa katika miaka ya 1890 kiasi cha Ujerumani kutangaza zawadi kwa yeyote atakeleta kichwa chake. Inaaminika kwamba alijitoa uhai mwenyewe mnamo 1898, badala ya kuingia izara ya kukamatwa, wakati alipokuwa akijificha katika pango lililozungukwa na wanajeshi wa Ujerumani. Miongo miwili baadaye, mjadala kuhusu hatma ya fuvu hilo uligubika majadiliano ya wanadiplomasia ambao kwa miezi kadhaa walishindana kuhusu makubaliano ya vita hivyo v...