Chifu Mkwawa: Shujaa aliyewaongoza Wahehe kupinga utawala wa kikoloni Afrika mashariki
Fuvu la Chifu Mkwawa limewekwa ndani ya sanduku la kigae katika jumba la ukumbusho la Mkwawa huko Kalenga, Tanzania ya kati.
Lakini kama taji, awali lilitundikwa katika nyumba ya afisa wa kikoloni huko Bagamoyo, kabla ya kuondolewa na kupelekwa Ujerumani - mkoloni wa mji huo - mwanzo mwa karne ya 20.
Fuvu hilo lilitumika kuwatishia Wahehe, ambao waliongozwa na shujaa huyo katika vita vya kupinga utawala wa kikoloni wa Ujerumani.
Na ufanisi wake ulikuwa ni mkubwa katika miaka ya 1890 kiasi cha Ujerumani kutangaza zawadi kwa yeyote atakeleta kichwa chake.
Inaaminika kwamba alijitoa uhai mwenyewe mnamo 1898, badala ya kuingia izara ya kukamatwa, wakati alipokuwa akijificha katika pango lililozungukwa na wanajeshi wa Ujerumani.
Miongo miwili baadaye, mjadala kuhusu hatma ya fuvu hilo uligubika majadiliano ya wanadiplomasia ambao kwa miezi kadhaa walishindana kuhusu makubaliano ya vita hivyo vikuu vya kwanza.
Lakini kwanini fuvu la shujaa huyo aliyepinga utawala wa kikoloni linatajwa katika 'Mkataba wa Versailles'?
'Treaty of Versailles' kama ulivyofahamika ulioidhinisha muungano wa mataifa na kueleza fidia iliyostahili kulipa Ujerumani kwa kuanzisha mzozo, ni waraka wenye maelfu ya maneno ulio na jumla ya vipengee 440.
Waraka huo uliosainiwa tariban karne moja iliyopita, ulitoa mtazamo mpya Ulaya kufuatia vita vya kwanza vya dunia.
Fuvu hili linatupatia fursa ya kujivunia watu waliopinga wakoloni"
Eric Jordan
Jumba la ukumbusho Mkwawa Kalenga
Majadiliano ya mvutano
Mamia ya wanadiplomasia kutoka kote duniani, waliokusanyika katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, waliandika wakifuta rasimu ya waraka huo. Mvutano uliokuwepo katika utaratibu huo huenda ulitoa fursa kwa vipengee kujumuishwa ndani ya waraka huo kuhusu fuvu la chifu Mkwawa - kwa ukubwa iligusia shukrani kwa Horace Byatt, kiongozi wa kikoloni wa Uingereza aliyekuwepo Afrika mashariki.
Mkataba huo ulisainiwa katika kasri la Versailles
Mwanahistoria Jeremiah Garsha amepata barua ambayo Byatt aliituma siku tatu baada ya kumalizika vita hivyo vikuu mnamo Novemba 1918, iliyoshinikiza fuvu hilo lirudishwe Tanzania kutoka Ujerumani, akieleza kwamba ni jambo "litakalowaridhisha" jamii ya Wahehe na kutoa "ushahidi wa kweli machoni mwa jamii hiyokwamba utawala wa Kijerumani umevunjwa kabisa".
Huenda alikuwa na dhamira nyingine - kuonyesha kwamba Uingereza, iliyodhibiti maeneo yaliotawaliwa na Ujerumani Afrika mashriki - sasa ipo uongozini. Lakini wakati viongozi hao wanne wa mataifa makuu yenye nguvu waliposikiliza pendekezo hilo, hawakushawishika.
Bwana Garsha amepata maandishi ya mojawapo wa mikutano mnamo Februari 1919 ambapo ilisemekana kuwa athri kwa Wahehe "haitoshi kujumuishwa kuhusu fuvu hilo kwenye mkataba wa amani".
' Ukubwa wa udadisi'
Pengine huo ndio ungepaswa kuwa mwisho wake, lakini baadih katika kambi ya Uingereza akiwemo katibu Kanali Viscount Milner, walivutiwa sana na suala hilo na kuona fursa katika kifungu hicho cha mkataba kilichogusia kuhusu kuwafidia na kuomba radhi kwa waliokosewa.
Jina kamili la Chifu Mkwawa:
Alizaliwa 1855 na akaitwa Ndesalasi, maana yake "Mtundu au Mdadisi"
Katika utu uzima aliitwa Mtwa Mkwava Mkwavinyika Mahinya Yilimwiganga Mkali Kuvago Kuvadala Tage Matenengo Manwiwage Seguniwagula Gumganga, maana yake: "Mtawala, mtekaji wa nyika, mkali kwa wanaume mpole kwa wanawake asiyetabirika, alieshindikanika, mbabe mwenye nguvu udongo pekee ndio utakomuweza"
Alipewa jina hilo mnamo 1887, baada ya vita na kabila la Wangoni kutoka Songea
Wajerumani walilifupisha jina hili na kumuita Mkwawa, wakilitamka "Mkwava" - lakini sasa linatamkwa kama linavyoandikwa
Baadhi ya mataifa yalitaka Ujerumani irudishe baadhi ya kumbukumbu na Bwana Mr Garsha anaeleza kwamba kuwa ni namna Milner alivyolifafanuwa fuvu hilo "ukubwa wa udadisi" ulioruhusu fuvu hilo kutazamwa kama kitu cha sanaa.
Na kwa hivyo chini ya kifungu "maagizo maalum" na yaliogubikwa katikati ya maagizo kutoka Ufaransana Ubelgiji kuna kifungu cha 246 kisemacho: "Katika miezi sita… Ujerumani itarudisha kwa serikali ya ufalme wa Uingereza fuvu la Sultan wa Mkwawa, lililoondoshwa kutoka himaya ilokuwa chni ya utawala wa Ujerumani Afrika mashariki na kupelekanchni Ujeurmani."
Hatahivyo, fuvu hilo halikurudishw akatika miezi sita - ilichukua miaka 35 kwa hilo kufanyika.
Hapo awali Ujerumani ilikana kuwa ina fuvu la Chifu Mkwawa, lakini lilisalia kuwa kiashiria muhimu kwa Uingereza waliochataka kukitumia kwa maslahi yake.
Kwahivyo ilipogunduliwa kuwa fuvu hilo lipo katika mji wa Bremen Ujerumani katika miaka ya 1950, gavan wa Uingereza wa iliyokuwa Tanganyika, Edward Twining, alikuwa mwepesi kuchukua hatua.
Alikwenda kuchunguza masalio ya binaadamu yaliokusanywa na aliligundua fuvu hilo katika mkusanyiko huo wa kumbukumbu zilizohifadhiwa wakati wa vita viku vya kwanza.
Natumai kwamba wewe na watu wenu mutaendelea kumtii Malkia Elizabeth II na warithi wake."
Edward Twining, Gavana wa Uingereza Tanganyika
Akimkabidhi mjukuu wa Shujaa Mkwawa, mfalme Adam Saapi mnamo 1954
Twining alichukua fursa kwa kupigia upatu ushujaa wa Mkwawa - kiongozi huyo ambaye mnamo 1891 aliongoza ushindi wa wanajeshi wake kwa kutumia mikuki dhidi ya Wajerumani, ambapo walifanikiwa kuwaua wanajeshi 300 na kuchukua bunduki zao katika vita huko Lugalo.
Jamii ya Wahehe walikuwa wakishinikiza vita Kaskazini na walifanikiwa kushinda udhibiti wa maenoe zaidi Afrika mashariki katika nusu ya pili ya karne ya 19 wakati Ujerumani ikjaribu kudhibiti maeneo.
Miaka mitatu baadaye, Ujerumani ulikusanay wanajeshi wake, mara hii ikileta vifaru vya nguvu kukishinda nguvu kikosi cha Wahehe.
Lakini Mkwawa aliepuka kukamatwa kwa miaka minne ya ziada, mpaka mwisho alipozingirwa na wanajeshi katika pango alikojificha ambapo aliamua kujitoa uhai.
Twinning alilitekeleza hilo kwa kupigizia kuwa: "Natumai kwamba wewe na watu wenu mutaendelea kumtii Malkia Elizabeth II na warithi wake."Alisema akimkabidhi mjukuu wa Shujaa Mkwawa, chifu Adam Saapi mnamo 1954
Kwake Twining utiifu huo ulisambaa katika kukipigani kikosi cha Uingereza wakati wa ukoloni kilichojulikana kama King's African Rifles (KAR) - kikosi cha jeshi na walinzi kilichosajiliwa kutoka Afrika mashariki.
"Itasikitisha sana iwapo WaHehe watalegea na kupoteza uwezo wao wa kupigana vita," aliongeza.
Afisa wa usajili kutoka KAR alikuwepo katika sherehe hiyo ya ukabidhi wa fuvu, taari kuwasjali vijana 70.
Bwana Garsha ameiambia BBC kwamba hili lilifanyika mnamo 1954 wakati vuguvugu la Mau Mau lilikuwa likiendelea katika nchi jirani Kenya - na wanajeshi wa KAR walitumika katika msako mkali.
Chifu Sappi apigwa picha karibu na fuvu la babu yake siku liliporudishwa
Lakini mnamo 1954 ni mwaka ambapo pia Julius Nyerere aliunda Muungano wa Afrika wa Tanganyika ambao ulifanikiwa kujinyakulia uhuru kutoka Uingereza mnamo 1961.
Licha ya kwamba kwa wakati mmoja wakoloni walitarajia fuvu la Shujaa Mkwawa litawasaidia kwa manufaa yao, lilitumika kama kiashiria cha Tanzania ilio huru na inayojivunia - na mpaka leo lipo katika jumba la ukumbusho huko Kalenga.
Maoni