Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tetesi za Soka Ulaya leo Alhamisi



Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amefutilia mbali uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona, Philippe Coutinho, 27, ambaye aliondoka Anfield kwa kima cha Ā£142m mwaka 2018. (ESPN)

Paris St-Germain imekubali kulipa Ā£28m kumsajili kiungo wa kimataifa wa Senegal Idrissa Gueye, 29, kutoka Everton. (Mail)


Toffees wanaendelea kushauriana na Crystal Palace kuhusu usajili wa nyota wa kimataifa wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, kwa pauni Ā£80m. (Sky Sports)

Tottenham imewasiliana na Juventus kuhusu usajili wa nyota wa kimataifa wa Argentina international mshambuliaji Paulo Dybala, 25, ambaye bei yake anayekadiriwa kuwa Ā£80m. (Evening Standard)


Paul Dybala

Manchester United wameomba kufahamishwa kuhusu hatma ya mchezaji Christian Eriksen, 27, wa Tottenham. Kandarasi ya nyota huyo wa kimataifa wa Denmark amesalia na mwaka mmoja kukamilika na huenda akauzwa kwa pauni milioni 70. (Mail)


United pia inamlenga mshambuliaji wa Lille na nyota wa kimataifa wa Ivory Coast Nicolas Pepe, 24, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa Ā£70m, kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku endapo atajiunga na Inter Milan. (Times)


Romelu Lukaku aliifungia United mabao 15 msimu uliopita

Kiungo wa kati wa Kimataifa wa Serbia na Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 24, amewaambia wachezaji wenzake kuwa ataondoka klabu hiyo msimu huu licha ya tetesi huendaakajiunga na Manchester United. (Il Tempo via Express)



Chelsea na West Ham wanapania kumsajili kwa mkopo winga wa Portsmouth Leon Maloney, 18 ambaye ameifungia Pompey academy mabao 26 msimu uliopita. (Sun)

Wolfsburg na RB Leipzig wanataka kumsajili kwa mkopo winga wa Arsenal wa miaka 18 Muingereza Emile Smith Rowe. (Independent)


Emile Smith-Rowe

Crystal Palace na Aston Villa wanataka kumsajili kiungo wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland anayecheza safu ya mashambulizi Jonathan Afolabi ambaye aliondoka Southampton mwisho wa msimu uliopita. (Football.London)

Sheffield United ambao wamepandishwa daraja kushiriki ligi kuu ya Premia wanatafakari uwezekano wa kumnunua kipa wa zamani wa kimataifa wa England Joe Hart, 32, kutoka Burnley. (Mail)


Kipa wa Burnely Joe Hart

Villa wanashauriana na kipa wa Juventus, Mtaliano Mattia Perin baada ya uhamisho wake Ā£13m kwenda Benfica kugonga mwamba baada ya kukosa uchunguzi wa kiafya. (Football Italia)

Barcelona wameweka dau la Ā£24m kumnunua mlinzi wa Real Betis na Uhispania Junior Firpo. (Sport - in Spanish)

Tetesi Bora Jumatano

Paris St-Germain wameishinda Juventus katika kinyang'anyiro cha kumsaini mlinzi wa Tottenham Danny Rose, 29, na wanaamini watafikia mkataba wa pauni milioni 20 kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa England . (Sun)

Naibu mwenyekiti mkuu wa Manchester United, Ed Woodward yuko mbioni kushughulikia suala la usajili wa wachezaji wapya, zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya muda wa mwisho wa uhamisho wa wachezaji kukamilia. (ESPN)



Woodward ana matumaini ya kukamilisha mchakato wa usajili wa mlinzi wa timu ya taifa ya England na klabu ya Leicester City, Harry Maguire, 26, na mchezaji wa safu ya kati wa Newcastle Sean Longstaff, 21. (London Evening Standard)


Mlinzi wa Leicester City, Harry Maguire

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp bado anapania kumnunua mchezaji mwingine mmoja msimu huu. (Liverpool Echo)

Mchezaji wa safu ya kati wa Sporting Lisbon na Ureno Bruno Fernandes, 24, amesema kuwa ataendelea kucheza katika ligi kuu ya Ureno licha ya tetesi zinazomhusisha na uhamisho wa kwenda Manchester United. (Mirror)


Bruno Fernandes

Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery ana wiki mbili kuamua ikiwa atamuachilia winga wa England wa chini ya miaka-21 Reiss Nelson, 19, kujiunga na Hertha Berlin kwa mkopo msimu ujao. (Sun

Tottenham wanakaribia kumsaini kiungo wa kati wa Real Betis Muargentina Giovani lo Celso, 23, kwa kima cha pauni milioni 45. (Sun

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...