
Real Madrid wana imani watafanikiwa kumsajili kiugo wa kati Mfaransa Paul Pogba kutoka Manchester United msimu ujao. (ESPN)
Bayern Munich wameanza mazungumzo na Manchester City kuhusu usajiliwa wa winga wao wa miaka 23 Mjerumani Leroy Sane, amabaye thamani yake inakadiriwa kuwa Ā£90m. (Mirror)
Romelu Lukaku, 26, amesafiri nyumbani Ubelgiji siku ya Ijumaa kufanya mazungumzo na ajenti wake huku Inter Milan wakikaribia kufikia mkataba wa Ā£70m kumnunua kuingo huyo wa safu ya ushambulizi kutoka Manchester United. (Daily Mail)

Romelu Lukaku akiwa mazoezini na wachazaji wenzake
Mmiliki wa Newcastle Mike Ashley amesema chamsingi ni maishani ni "pesa kwanza kisha klabu baadae" kwa maneja wake wa zamani Rafael Benitez, na kuongeza kuwa "ni vigumu" kuendelea kumng'ang'ania raia huyo wa Uhispania. (Mail)
Atletico Madrid wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Colombia James Rodriguez, 28, kutoka kwa mahasimu wao Real Madrid. (Independent)

Mshambuliaji wa Ureno Rafael Leao, 20, anajiandaa kuondoka Lille kwenda AC Milan kwa mkataba wa euro milioni 35 - utakaojumuisha 20% ya makataa ya kumuuza. (RMC Sport)
Bournemouth wanapania kuipiku Brighton katika usajili wa Ā£15m wa kiungo wa kati wa Huddersfield Philip Billing, 23. (Sun)
Swansea City wanakabiliwa na hatari ya kumkosa mchezaji wa safu ya kati wa Chelsea mwenye umri wa miaka 22-Kasey Palmer. (Wales Online)

Kasey Palmer
Panathinaikos wanatafakari uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Ivory Coast anayechezea Celtic Kouassi Eboue, 21. (Daily Record)
Bekiwa Real Madrid wa miaka 22 Mhispania Jesus Vallejo anafanyiwa vipimo vya kimatibabu Wolves kabla ya kuhamia klabu hiyo kwa mkopo. (Talksport
Maoni