Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya FIFA

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 10.07.2018

Beki wa zamani wa Real Madrid Michel Salgado anaamini mshambuliaji wa Tottenham na Uingereza Harry Kane, 24, ndiye anayelengwa na klabu hiyo msimu huu baada ya mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 26. (Talksport) Chelsea inajaribu kuipiku Manchester City katika kumsaini kiungo wa kati wa Lazio na Itali Jorginho, 26. (Manchester Evening News) City pia imembishia hodi kiungo wa kati wa Real Madrid na Croatia Mateo Kovacic, 24, huku wakiwa na wasiwasi kuhusu kumtia mkobani Jorginho. (Mirror) Mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 29, anatarajiwa kusalia na klabu hiyo licha ya kuhusishwa na uhamisho (Bild) Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Roma Monchi anasema kuwa ataangazia maombi ya kumuuza kipa wa Brazil Alisson lakini kufikia sasa hakuna klabu iliowasilisha ombi la kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (FourFourTwo) Manchester United na Real Madrid wamekutana na maafisa kutoka Lazio kujadili uhamisho wa kiungo wa...

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

SHERIA 17 ZA SOKA ======================= Mchezo wa soka ni moja ya michezo maarufu sana duniani na ni biashara kubwa sana katika ulimwengu wa michezo na ukitaka kuamini hili angalia makampuni yaliyowekeza katika kudhamini soka – ni makampuni makubwa makubwa yenye hadhi ya kitaifa na kimataifa. Kwa kuzingatia aina hii ya wadhamini, waendeshaji wa mchezo wa soka, wameweka kanuni na miongozo ya kufuatwa ili kuhakikisha kuwa wale wanaowekeza pesa zao wanaona thamani ya uwekezaji wao. Kwa hiyo soka kama ilivyo katika michezo mingine inazo kanuni na tutajadili kanuni moja baada ya nyingine kama zilivobainishwa katika muongozo wa FIFA unaojulikana kwa jina la Law of the Game. Sheria Namba 1: Dimba ============== NYASI - Dimba la soka litakuwa la nyasi asilia au bandia kulingana na kanuni za masindano na nyasi hizo lazima ziwe za rangi ya kijani. Kwa dimba la nyasi bandia na kama mchezo unaochezwa utakuwa wa kutambuliwa na FIFA, basi nyasi hizo bandia lazima zikidhi viwango maalumu ...