Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya LONDON

Waabiri ndege kisiri 'stowaway' huponea?

Mshukiwa aliyeabiri ndege kisiri inaaminika ameanguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways  kutoka Nairobi kuelekea Heathrow, na kuanguka katika bustani moja huko kusini mwa London Lakini ni mara ngapi visa kama hivyo huhuhudiwa na hali huwa vipi wakati wa safari za aina hiyo? Ni mara ngapi visa hivi hutokea? Licha ya kwamba sio jambo la kawaida, hii sio mara ya kwanza kwa mtu kuingia katika sehemu za ndege wakati ndege hiyo ikisafiri na kujificha wakati wa safari ya kuelekea Uingereza. mwili ulipatikana katika bustani ilioko Offerton Road huko Clapham Kati ya Januari 2004 na Machi 2015, watu sita walioingia kwa siri katika ndegekatika uwanja wa ndege Uingereza walipatikana kwa mujibu wa  takwimu za hivi karibuni za shirika la viwanja vya ndege (CAA ). Mwingine mmoja alipatikana katika ndnai ya ndege ya Uingereza katika uwanja wa ndege ng'ambo. Takwimu kutoka shirika la viwanja vya ndege Marekani zimeashiria kuwa watu 96 wamewahi kujificha katika sehemu za ndege ...

NDEGE YA KENYA YA DODOSHA ABIRIA UINGEREZA

Mwili wa mtu aliyeabiri ndege ya Kenya Airways kisiri 'stowaway' waanguka London ''Mtu'' huyo alianguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka mjini Nairobi Jumapili mchana Mwili wa mtu anayeshukiwa kuabiri ndege ya Kenya Airways kisiri 'stowaway' umeanguka ndege hiyo ikielekea kutua katika uwanja wa ndege wa Heathrow mjini London. Mwili huo - unaoaminiwa kuwa wa mwanamume - ulipatikana umeanguka katika bustani ya Clapham siku ya Jumapili. Polisi wanasema mtu huyo alianguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka mjini Nairobi. Mkoba, maji na vyakula vilipatikana katika eneo lililo chini ya gia ya ndege wakati ilipokua ikutua. Polisi wa wa jiji la London wamesema mwili huo utafanyiwa uchunguzi kubaini kilichosababisha kifo chake na kwamba kifo chake. Kenya Airways imesema kuwa ndege hiyo imefanyiwa uchunguzi na hakuna hitilefu yoyote ilioripotiwa. Msemaji wa shirika la ndege hiyo amesem...