Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England Manchester City wamepangiwa kucheza na klabu ya Schalke ya Ujerumani katika hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya droo kufanywa. Manchester United wamekabidhiwa miamba wa Ufaransa Paris Saint Germain. Mabingwa hao watetezi wa ubingwa Ufaransa hawajashindwa msimu huu ligini nyumbani ambapo wanaongoza wakiwa na alama 44 kutoka mechi 16. Wana washambuliaji nyota kama vile Neymar, Kylian Mbappe na Edison Cavani. Walimaliza viongozi Kundi C, kundi ambalo lilikuwa na Liverpool, Napoli na Red Star Belgrade katika hatua ya makundi. Lakini walishindwa na Liverpool uwanjani Anfield. United hawajawahi kukutana na Paris St-Germain katika michuano ya Ulaya. Hata hivyo, mashetani hao wekundu hawajawahi kushinda na klabu yoyote kutoka Ufaransa katika michuano ya Ulaya tangu mwaka 2005. Droo kamili: Manchester United v PSG Schalke v Manchester City Atletico Madrid v Juventus Tottenham v Borussia Dortmund Lyon v Barcel...