Marekani inahofia makombora mapyaya Urusi Urusi imejiondoa katika mkataba wa kupinga uundaji wa makombora ya masafa marefu uliyofikiwa enzi ya vita baridi kufutia uamuzi sawa na huo uliyochukuliwa na Marekani. Rais Vladimir Putin amesema taifa hilo litaanza kuunda makombora mapya. Marekani ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiilaumu Urusi kwa kukiuka mkataba huo ilitangaza kusitisha rasmi wajibu wake siku ya Ijumaa. Mkataba huo uliyofikiwa kati ya Marekani na muungano wa Sovieti, USSR na kutiwa saini mwaka 1987 ulipiga marufuku mataifa yote dhidi ya matumizi ya makombora ya masafa mafupi na yale ya kadri. "Washirika wetu wa Marekani wametangaza kusitisha wajibu wao katika mkataba huo nasi pia tunafuata mkondo wao,"alisema Bw. Putin siku ya Jumamosi. Urusi ilirusha kombora katika mazoezi ya kijeshi Katibu mkuu wa muungano wa kijeshi wa mataifa ya magharibi Nato, Jens Stoltenberg amaiambia kuwa: "Washirika wote [Ulaya] yameunga mkono hatua ya Marekani kwasababu Ur...