Mbabane Swallows wamkabidhi Kinnah Phiri mtihani wa Simba Kocha wa zamani wa Mbeya City, Kinnah Phiri amekabidhiwa jukumu la kuiongoza klabu ya Mbabane Swallows katika mechi dhidi ya Simba. Phiri amepewa jukumu hilo la muda mfupi kutokana na kocha mkuu wa Mbabane Swallows, Thabo Vilakati kutumikia adhabu ya kifungo cha mechi nne kutoka CAF kwa kosa la kumpiga muokota mpira. Simba itapambana na Mbabane Swallows katika mechi ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa Jumatano.