Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya PERU

Maandamano baada ya rais wa zamani Peru kuachiliwa

MTEULE THE BEST Maandamano baada ya rais wa zamani Peru kuachiliwa Rais wa Peru Pedro Pablo Kuczynski amemsamehe rais wa zamani Alberto Fujimori katika misingi ya kiafya katika hatua ambayo imezua maandamano makali. Fujimori, 79, ambaye anatumikia kifungo cha miaka 25 jela kwa ukiukaji wa haki za binadamu na ufisadi alihamishwa kutoka gerezani kwenda hospitalini kutokana na sababu za kiafya siku ya Jumamosi. Bw Kuczynski alikana kuwa kumsamehe kwake kulikuwa ni sehemu ya makubaliano ya chama chake kuzuia kura ya kutokuwa na imani naye. Polisi katika mji mkuu Lima walipambana na waandamanaji baada ya kuibuka kwa habari hizo. Hata hivyo wafuasi wa Fujimor ambaye aliongoza Peru kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2000 walisherehekea nje ya hospitali ya serikali ambapo alikuwa akipata matibabu. Anapendwa na baadhi ya rais wa Peru kwa kuwamaliza waasi wa Mao lakini wakosoaji wake wanamtaja kuwa mtawala wa kiimla