Sanchez anahusishwa na uhamisho wa Manchester City mwezi huu. Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa uamuzi wake wa kumchezesha Alexis Sanchez kama mchezaji wa ziada dhidi ya Chelsea siku ya Jumatano hauna uhusiano na uvumi kuhusu uhamisho wake na kusisitiza hamu yake ya mshambuliaji huyo kusalia katika kabu hiyo. Mshambuliaji huyo wa Chile ambaye kandarasi yake inakamilika mwezi Juni aliingia katika kipindi cha pili katika nusu fainali ya kombe la Carabao mkondo wa kwanza mbapo timu hizo zilitokare sare tasa. Sanchez anahusishwa na uhamisho wa Manchester City mwezi huu. ''Nataka asalie kwa kipindi kirefu'',alisema Wenger. ''Sina tatizo iwapo atasaini kandarasi mpya nasi iwe sasa au mwezi Juni''. Lazima ukubali wakati unapocheza mechi nyingi na Sanchez hucheza kila mechi, na kwamba wanapopimzika katikati ya msimu huwasaidia kidogo. Licha ya utata unaokumba hatma ya Sanchez, Wenger haamini kwamba Sanchez anataka kuondoka....