Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya CAF AWARD

SIMBA KUJUA MBIVU AMA MBICHI 28/12/2018 CAIRO

mteulethebest Draw ya makundi ya kombe la klabu bingwa barani Afrika (Caf Champions League) itafanyika Cairo Misri siku ya Ijumaa December 28 na klabu ya Simba itawakilishwa na mwenyekiti wa bodi Swed Kwabi. -Shirikisho hilo limepanga pot 4 kila pot ina timu 4 na kila pot itatoa timu moja kwenye kundi moja. Pot hizo zimepangwa kulingana na Parfomance ya klabu kwa miaka mitano iliyopita kwa Caf Champions League na Caf Confederation Cup. -Pot 1 ina vilabu vya TP Mazembe (DR Congo) yenye pointi 66, Al Ahly (Egypt) yenye pointi 62, Wydad Casablanca (Morocco) yenye pointi 51 na Esperance de Tunis (Tunisia) yenye pointi 45. -Pot 2 ina vilabu vya Mamelodi Sundowns (South Africa) yenye pointi 40, AS Vita Club (DR Congo) yenye pointi 29, Horoya (Guinea) yenye pointi 19 na Club African (Tunisia) yenye pointi 12. -Pot 3 ina vilabu vya ASEC Mimosas (Ivory Coast) yenye Point 8.5, Orlando Pirates (South Africa) yenye pointi 8, FC Constantine (Algeria) na FC Platinum (Zimbabw...

Serengeti Boys” itashiriki kwenye mashindano maalumu ya CAF na UEFA

Shirikisho la Soka Tanzania TFF limetangaza kuwa Timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania U17 “Serengeti Boys” itashiriki kwenye mashindano maalumu ya maandalizi ya Afcon U17 yatakayofanyika Antalya nchini Uturuki mapema mwakani. Kikosi cha Serengeti Boys Kwa mujibu wa taarifa ya TFF kupitia tovuti yake, mashindano hayo yameandaliwa na Shirikisho la Soka barani  Afrika CAF kwa ushirikiano na Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA, ambapo yanatarajia kuanza Februari 22,2019 mpaka Machi 2,2019 na kushirikisha jumla ya timu 12 kutoka Afrika na Ulaya. Mbali na Serengeti Boys, nchi nyingine za Afrika zitakazoshiriki katika mashindano hayo ni pamoja na Angola, Morocco, Cameroon, Uganda, Nigeria, Senegal na Guinea ambazo zitaungana na timu nne kutoka bara la Ulaya. Serengeti Boys imewasili nchini jana Desemba 17 ikitokea nchini Botswana ambako ilialikwa kushiriki mashindano ya mataifa ya kusini mwa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, ambako imefanikiwa kurudi na ubingwa w...

Simba yaicharaza Mbabane Swallows FC Kipigo cha mbwakoko

Timu ya Simba imeanza vizuri kwenye mashindano ya Ligi ya mabingwa Afrika kwakuapiga Mbabane Swallows FC 4-1 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.  Mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco dakika ya 7 akimalizia pasi ya Nicolus Gyan kisha akafunga bao la pili dakika ya 32 kwa mkwaju wa penati baada ya Emmanuel Okwi kuchezewa rafu na mlinda mlango wa Mbabane.  Mbabane waliweza kutikisa nyavu za Simba dakika ya 24 lililofungwa na Guevane Nzambe na kufanya kipindi cha pili kumalizika kwa bao 2-1.  Simba walirejea kwa kasi kipindi cha pili na kufanikiwa kufanya mashambulizi na wakafunga bao la 3 lililofungwa na Meddie Kagere dakika ya 83 baada ya mlinda mlango wa Mbabane kuteleza akiwa na mpira kisha dakika ya 90 Clatous Chama alifunga bao la 4 akimalizia pasi ya Hassan Dilunga.  Simba watatakiwa wasiruhusu bao wakienda ugenini ili waweze kusonga mbele katika hatua ya michuano hii kwa kuwa Mbabane sio timu ya kubeza

WATAMBUE WACHEZAJI 30WALIO CHAGULIWA KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRICA

Walioteuliwa katika orodha hiyo ni: 1. Ali Maaloul (Tunisia na Al Ahly) 2. Bertrand Traore (Burkina Faso na Lyon) 3. Cedric Bakambu (DR Congo na Villareal) 4. Christian Atsu (Ghana na Newcastle) 5. Christian Bassogog (Cameroon na Henan Jianye) 6. Denis Onyango (Uganda na Mamelodi Sundowns) 7. Eric Bailly (Cote d'Ivoire na Manchester United) 8. Essam El Hadary (Egypt na Al Taawoun) 9. Fabrice Ondoa (Cameroon na Sevilla) 10. Fackson Kapumbu (Zambia na Zesco) 11. Jean Michel Seri (Cote d'Ivoire na Nice) 12. Junior Kabananga (DR Congo na Astana) 13. Karim El Ahmadi (Morocco na Feyenoord) 14. Keita Balde (Senegal na Monaco) 15. Khalid Boutaib (Morocco na Yeni Malatyaspor) 16. Mbwana Samata (Tanzania na Genk) 17. Michael Olunga (Kenya na Girona) 18. Mohamed Salah (Egypt na Liverpool) 19. Moussa Marega (Mali na Porto) 20. Naby Keita (Guinea na RB Leipzig) 21. Percy Tau (South Africa na Mamelodi Sundowns) 22. Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon na Borussia Dortmund) ...