Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya SPIKA

Spika Ndugai ataja kosa kubwa analoshtakiwa Masele

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele, hawezi kukaidi tena agizo la kutakiwa kufika Kamati ya Maadili baada ya kuitwa na Spika huyo kwa mara ya pili. Spika wa Bunge Job Ndugai. Akizungumza na waandishi wa habari Spika Ndugai amesema suala la Bunge kumuita Masele halihusiani na matukio yaliyotokea Afrika Kusini bali ni kwa sababu ya mambo aliyofanya nyumbani. Spika Ndugai amesema " ameitwa kwa mambo ya hapa nyumbani ya utovu wa nidhamu, anaunganisha hilo na matendo anayoyafanya huko, lakini hatujamuita kwa mambo ya South Afrika Watanzania watulie baada ya muda zitaletwa bungeni kila mtu atasikia kuhusu anatuhumiwa nini na majibu yake yalikuwa nini na wataelewa kama ameonewa au hajaonewa ." " Stephen Masele hawezi kukaidi zaidi kwa sababu ni lazima arudi Tanzania, labda sababu awe mkimbizi na  akirudi Tanzania lazima aje Kamati ya Maadili, ni wito wa kisheria tunachomuitia ni tabia yake uchonganishi wa viongozi, kwa sasa hatu...

Ndugai awachimba mkwara Wabunge wa 'hapana'

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewatahadharisha Wabunge wake kwamba endapo wataipigia kura ya hapana Bajeti ya Serikali ya mwaka 2018/19, Rais atalivunja Bunge hilo huku akiwakumbusha wengine wanaweza wasirudi kwenye mjengo huo. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo wakati akiwakumbusha wabunge kazi waliyonayo leo itakapofika saa 11 jioni  ambayo itakuwa kupiga kura ya kuipitisha bajeti. “Endapo mlio wengi mtaikataa Bajeti ya Serikali, bunge hili Rais atalivunja haraka. Na baadhi yenu, mkirudishwa majimboni hamrudi kwa hiyo akili za kuambiwa changanya na zako .” amesema Spika Ndugai. B Mbali na hayo Ndugai amewasisitiza wabunge wote kuwapo bungeni ifikapo saa 11  na kuwakumbusha kuwa kura haipigwi kwa jambo moja, bali ni kwa mfuko wote wa bajeti. Wabunge wanatarajia kupigia kura bajeti ambapo Serikali inatarajia kukusanya na kutumia TSh32...