Ndugai awachimba mkwara Wabunge wa 'hapana'


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewatahadharisha Wabunge wake kwamba endapo wataipigia kura ya hapana Bajeti ya Serikali ya mwaka 2018/19, Rais atalivunja Bunge hilo huku akiwakumbusha wengine wanaweza wasirudi kwenye mjengo huo.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai


Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo wakati akiwakumbusha wabunge kazi waliyonayo leo itakapofika saa 11 jioni  ambayo itakuwa kupiga kura ya kuipitisha bajeti.

“Endapo mlio wengi mtaikataa Bajeti ya Serikali, bunge hili Rais atalivunja haraka. Na baadhi yenu, mkirudishwa majimboni hamrudi kwa hiyo akili za kuambiwa changanya na zako.” amesema Spika Ndugai. B

Mbali na hayo Ndugai amewasisitiza wabunge wote kuwapo bungeni ifikapo saa 11  na kuwakumbusha kuwa kura haipigwi kwa jambo moja, bali ni kwa mfuko wote wa bajeti.

Wabunge wanatarajia kupigia kura bajeti ambapo Serikali inatarajia kukusanya na kutumia TSh32 trilioni katika mwaka wa fedha 2018/19 ikiwa ni ongezeko la TSh800 bilioni ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2017/18 ya TSh31.7 trilioni.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU