Baba Mzazi wa Michael Jackson  aaga dunia

Baba mzazi wa aliyekuwa Mfalme wa muziki wa Pop Michael Jackson mzee Joe Jackson amefariki Dunia kwa ugonjwa wa Saratani (Cancer) akiwa na umri wa miaka  89 mapema Jumatano leo


Baba mzazi wa aliyekuwa Mfalme wa muziki wa Pop Michael Jackson, Joe Jackson enzi za uhai wake.


Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka nchini humovimeeleza kuwa Bw. Jackson alikuwa akipambana na saratani ya kongosho .

Inadaiwa kuwa kwa miaka mingi, Jackson ambaye alizaliwa Julai 26, 1928, huko Fountain Hill, Arkansas alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya afya.

Joe alikuwa mzazi aliyefanikiwa sana kusimamia watoto wake katika historia ya muziki ambapo aliweza kujenga kundi la The Jackson 5, na kisha baadaye Michael na Janet Jackson kama wasanii solo.

Amefariki dunia ikiwa imepita siku moja tangu kumbukumbu ya miaka tisa ya kifo cha mwanae Michael ambaye alifariki dunia Juni 25 2009.

Jackson alikuwa na watoto 10 pamoja na Katherine ambaye ni mke wake wa zaidi ya miaka 60. 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU