Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wafikia makubaliano kuhusu uhamiaji

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamefikia makubaliano juu ya mpango wa uhamiaji, unaozitaka nchi wanachama kwa hiari kuanzisha vituo vya udhibiti kushughulikia wahamiaji waliookolewa baharini na kuanzisha vituo nje ya ulaya.


Mpango huo wa maelewano uliofikiwa mapema asubuhi ya leo unakuja baada ya majadiliano yaliyodumu kwa muda wa masaa zaidi ya 12, wakati viongozi hao walipokutana katikati mwa ongezeko la shinikizo la kutafuta ufumbuzi wa tatizo la uhamiaji, unaonekana kuhatarisha mustakabali wa umoja huo.


Mpango huo ni ushindi kwa Italia, inayoongozwa na waziri mkuu Giuseppe Conte, ambaye amekuwa akisukuma ajenda ya kugawana mzigo wa wahamiaji miongoni mwa nchi wanachama na hata kutishia kutumia kura yake ya turufu katika maamuzi ya mkutano huo wa kilele hadi pale viongozi wake wangefikia makubaliano ya pamoja juu ya uhamiaji. "Kwa hiyo naweza kusema kwa ujumla tunaweza kuridhika. Yalikuwa majadiliano ya muda mrefu lakini kuanzia leo Italia haiko peke yake," alisema Conte.


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akizungumza na waandishi wa habari


Serikali ya Conte ya mrengo mkali wa kulia imekuwa ikichochea mjadala wa uhamiaji Ulaya kwa kufunga bandari zake dhidi ya meli mbili zilizowaokoa wahamiaji katika wiki zilizopita, na kutaka mabadiliko makali katika sera ya Uhamiaji ya Ulaya.


Chini ya makubaliano haya mapya, nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zitaanzisha kwa hiari yake vituo vya udhibiti katika ardhi yake kushughulikia wahamiaji waliookolewa baharini.




Wale wanaostahili ulinzi wa kimataifa watagawanywa miongoni mwa nchi wanachama ambao watawachukua wahamiaji kwa hiari. Hii itaiondolea mzigo Italia, ambayo kwa sasa inashughilikia wahamiaji wengi waliokolewa kwenye bahari ya Mediterenia.


Muungano huo pia utafanyia kazi kwa haraka dhana ya majukwaa ya utengano wa kikanda yatakayokuwa ni vituo vya kushughulikia wahamiaji nje ya Ulaya, uwezekano mkubwa ikiwa ni Afrika ya kaskazini. Kwa hili Umoja wa Ulaya utahitaji idhini kutoka nchi nyingine zinazohusika.


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza na vyombo va habari


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameyasifu makubaliano hayo akisema licha ya kazi kubwa inayotakiwa kufanywa kabla ya ukanda huo haujafikia msimamo wa pamoja wa waomba hifadhi, lakini ana matumani kwamba kuanzia leo wataendelea na kazi.


"Tumekubaliana juu ya miongozo mitano lakini miwili bado inakosa mfumo wa pamoja wa Ulaya wa waomba hifadhi lakini nina matumaini baada ya leo tunaweza kuendelea kufanya kazi ingawa kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuunganisha mitazamo tofauti, alisema Merkel.


Merkel amekuwa chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa waziri wake wa mambo ya ndani Horst Seehofer ambaye amempatia muda wa mwisho wa hadi mwishoni mwa Juni ili apunguze idadi ya waomba hifadhi wanaiongia Ujerumani au ahatarishe serikali yake ivunjike.


Kansela wa Austria Sebastian Kurz amesema mpango huo utaiwezesha Umoja wa Ulaya kulinda mipaka yake kwasababu kwa mara ya kwanza kuna uwezekano wa kufunguliwa vituo nje ya Ulaya. Naye rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesifu mpango huo akiuita ufumbuzi wa Ulaya na matunda ya kazi ya pamoja. Amesema hii ni bora zaidi ya suluhisho la nchi moja moja, ambalo lisingefikiwa hata hivyo. Nchi hizo zimekubaliana kuongeza nyongeza ya yuro milioni 500 kuzisaidia nchi za afrika.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...