ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA
SHERIA 17 ZA SOKA ======================= Mchezo wa soka ni moja ya michezo maarufu sana duniani na ni biashara kubwa sana katika ulimwengu wa michezo na ukitaka kuamini hili angalia makampuni yaliyowekeza katika kudhamini soka – ni makampuni makubwa makubwa yenye hadhi ya kitaifa na kimataifa. Kwa kuzingatia aina hii ya wadhamini, waendeshaji wa mchezo wa soka, wameweka kanuni na miongozo ya kufuatwa ili kuhakikisha kuwa wale wanaowekeza pesa zao wanaona thamani ya uwekezaji wao. Kwa hiyo soka kama ilivyo katika michezo mingine inazo kanuni na tutajadili kanuni moja baada ya nyingine kama zilivobainishwa katika muongozo wa FIFA unaojulikana kwa jina la Law of the Game. Sheria Namba 1: Dimba ============== NYASI - Dimba la soka litakuwa la nyasi asilia au bandia kulingana na kanuni za masindano na nyasi hizo lazima ziwe za rangi ya kijani. Kwa dimba la nyasi bandia na kama mchezo unaochezwa utakuwa wa kutambuliwa na FIFA, basi nyasi hizo bandia lazima zikidhi viwango maalumu ...
Maoni