MTEULE THE BEST
Mohammed Morsi ahukumiwa kifungo cha maisha
Mahakama ya Misri imempatia kifungo cha maisha jela aliyekuwa rais wa Kiislamu Mohammed Morsi baada ya kukamilika kwa kesi yake ya upelelezi.
Ni miongoni mwa washtakiwa wanaoshtumiwa kwa kutoa nakala za siri kwa taifa la Qatar.Wakili wa Bw Morsi amesema kuwa aliwachiliwa huru kwa upelelezi lakini akapewa hukumu hiyo kutokana na kuliongoza kundi haramu.
Wengine ni waandishi wawili wa Aljazeera ambao walihukumiwa kifo wakiwa hawako mahakamani.
Maoni