MTEULE THE BEST
Kiongozi wa chama cha mashabiki wa kandanda nchini Urusi, anatimuliwa kutoka nchini Ufaransa kufuatia ghasia zilizotokea wakati wa mechi za kuwania kombe la taifa bingwa barani Ulaya, kati ya Urusi na Uingereza mjini Marseille.
Alexander Shprygin ni mmoja wa mashabiki 20 wa Urusi wanaotimuliwa kutoka Ufaransa.Walikamatwa siku ya Jumanne wakiwa safarini kutoka Marseille kwenda Lille kudhudhuria mechi kati ya Urusi na Slovakia
Kukamatwa kwao kuliikasirisha urusi iliyomuita balozi wa Ufaransa humo kupinga.
Chama hicho cha mashabiki kinachoongozwa na Shprygin kinaungwa mkono na serikali ya Urusi.
Mashabikia wa uingereza na Urusi walipamabana kabala ya na baada ya timu hizo kucheza siku ya Jumamosi.
Polisi wa Ufaransa walisema kuwa wahuni 150 wa Urusi waliopewa mafunzo ndio walihusika.