MTEULE THE BEST
P olisi nchini Zambia, wanasema kuwa wahamiaji 18 wenye asili ya Kisomali, wamefariki walipokuwa wakipelekwa kwa njia haramu kuingia katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
Walikuwa wamebebwa ndani ya bohari lililokuwa na mzigo wa Samaki.Kamishina mmoja mkuu wa polisi nchini Zambia Hudson Namachila, amesema kuwa lori hilo lilisimama ndani ya mpaka wa Kongo pale baadhi ya wahamiaji haramu waliokuwa wameishiwa na hewa, walipoanza kugonga gonga bohari hilo wakiwa ndani, kuwaashiria madereva wawafungulie ambao walikuwa wamekamatwa.
11 kati ya wasomali hao 44 tayari walipatikana kuwa wamekufa huku wengine saba wakifariki baadaye. 27 walionusurika kufa wametiwa mbaroni.