MTEULE THE BEST
Dar es Salaam. Matokeo ya awali yanaonyesha
kuwa Mwenyekiti wa Yanga anayetetea nafasi yake, Yusuph Manji anaongoza
kwa kura 1,468, na hakuna zilizomkataa, huku mbili zikiharibika.
Akizungumzia
uchaguzi huo ambao kura zimeendelea kuhesabiwa hadi asubuhi ya leo,
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha klabu hiyo, Jerry Muro amesema
Clemence Sanga anaongoza katika nafasi ya Makamu mwenyekiti kwa
kujikusanyia kura 1,428 dhidi ya mpinzani wake, Tito Osoro aliyekuwa
amepata kura 80.
Hadi taarifa
hizi zinapatikana kutoka Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es
Salaam, klabu hiyo ilikuwa inaendelea na mchakato wa kuhesabu kura za
wajumbe.Hata hivyo, Muro amesema matokeo kamili yatatolewa leo.
Maoni