MTEULE THE BEST
Mmoja wa wapuliza filimbi katika taasisi ya ulinzi wa taifa la Moscow Edward Snowden, ameeleza kuwa anamilki nyaraka za siri zinazoonyesha kuwa Osama Bin Laden yupo hai.
Snowden, ambaye anaishi kama mkimbizi nchini Russia ameeleza taarifa hizo ambazo hazijaweza kuthibitishwa kuhusu gaidi Osama Bin Laden alipokuwa akifanya mahonjiano na jarida la Moscow.
Edward Snowden anayeelza kuwa ana nyaraka zinazoonyesha kuwa Osama Bin Laden yupo hai.
Amesema kwamba, sio kwamba Osama yupo hai tu, bali anaishi maisha ya kifahari Bahamas.
“Nina
nyaraka zinazoonyesha kuwa Bin Laden bado yupo kwenye mfumo wa malipo
wa CIA. Osama anapokea zaidi ya dola 100,000 kwa mwezi, ambazo zimekuwa
zikisafirishwa na wafanyabiashara wakubwa na mashirika moja kwa moja
kwenda kwenye akaunti yake ya benki ya Nassau.”
Snowden aeleza kuwa shirika la kijasusi la
Marekani (CIA) lilidanyanga kuhusu kifo cha kiongozi wa zamani wa Al
Qaeda, wakati ukweli ni kuwa alisafirishwa kwa siri katika eneo ambalo
halikutajwa Bahamas.
“CIA kwa kushirikiana na
usalama wa taifa wa Pakistani waliidanganya dunia kuhusu kifo cha Osama.
Kwa vile kila mtu aliamini kuwa amekufa, hakuna aliyehangaika
kumtafuta, hivyo ilikuwa rahisi kwake kujificha. Bila ndevu (mzuzu) na
koti la kijeshi, hakuna mtu anaweza kumfahamu” alieleza Snowden.
Osama
Bin Laden ambaye alisemekana kuuawa na Jeshi la Majini la Marekani
mnamp 2 Mei 2011 imeelezwa kuwa yupo hai na anaishi maisha ya kufahari.
Edward Snowden alikuwa muajiriwa wa NSA mwaka 2013 baada ya kuwa alikuwa ameajiriwa na kampuni ya Dell na CIA. Mwezi wa sita mwaka huo alitoa nyaraka za siri za NSA kwa waandishi wa habari. Serikali ya Marekani ilimfunguliwa mashtaka baada ya kitendo hicho. Sasa amepewa hifadhi (asylum) nchni Moscow baada ya kutoroka Marekani kwa kosa la kuvujisha siri.