MTEULE THE BEST
Mbunge wa chama cha Leba nchini Ungereza
Mbunge wa chama cha Leba nchini
Ungereza Jo Cox ameaga dunia baada ya kupigwa risasi na kuchomwa kisu
akiwa kwenye mkutano katika eneo lake la ubunge kaskazini mwa uingereza.
Mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 52 aliyetajwa na majirani kama mtu asiye na marafiki amekamatwa na silaha kupatikana.
Mtu mmoja aliyeshuhudia alisema risasi ilifyatuliwa wakati Bi Cox aliingilia kati.
Kisha muuaji akaanza kumchoma kisu alipokuwa amelala chini.