Serikali ya Uingereza imependekeza mabadiliko makubwa katika uongozi wa shirika la utangazaji la BBC. Katibu wa wizara ya utamaduni bwana John Whittingdale, anapendekeza idhaa ya BBC kuongozwa na bodi maalum ambayo itakuwa na wanachama waliochaguliwa na BBC yenyewe wala sio serikali. Mabadiliko hayo hata hivyo yanaipa serikali nguvu zaidi jambo ambalo limetilia shaka uhuru wa BBC katika siku za usoni. Fedha za kufadhili shughuli za idhaa hiyo kongwe zitalindwa na hata kuongezwa maradufu na serikali ya Uingereza. Asilimia kubwa ya fedha zinazofadhili shughuli za BBC zinatokana na kodi inayotozwa kila mmiliki wa runinga nchini Uingereza. Serikali imependekeza kuiongezea BBC takriban pauni milioni 300 kufikia mwaka wa 2020. Ufadhili huo mkubwa unafuatia tathmini ya serikali inayotambua ushawishi mkubwa wa BBC kote duniani. Mapendekezo mengine ni kama ifuatavyo Ruwaza mpya ya BBC: "kuzingatia maslahi ya umma katika kila jambo, kutopendelea upa...